Apigwa faini ya milioni 5 kwa kutumia laini ya simu iliyosajiliwa na jina lisilo lake

Apigwa faini ya milioni 5 kwa kutumia laini ya simu iliyosajiliwa na jina lisilo lake

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ernest Lwila (30) kulipa faini ya TSh5 milioni au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani, baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine.

Pia, mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa huyo katika shtaka la kuchapisha taarifa za uongo na kuzisambaza mtandaoni bila leseni baada ya kutomkuta na hatia.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Mlowo, wilayani Mbozi, ameshindwa kulipa faini hiyo, hivyo amepelekwa gerezani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Desemba 2, 2024 na Hakimu Rahim Mushi, baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 10 na vielelezo saba.

Sikujua hili kosa liko serious kiasi, limezidi hadi wabadhirifu wa mali za umma wanaohukumia kwenda kufanya usafi kwenye maeneo ya umma.
 
Back
Top Bottom