Apigwa na mumewe kisa pesa ya kununua sukari robo!

Apigwa na mumewe kisa pesa ya kununua sukari robo!

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Hiki kisa kinaweza kuwa kinachekesha ila kina funzo ndani yake!

Mama mmoja mwenye umri wa miaka 30 na watoto watano, amejikuta akitandikwa NGUMI ZA CHEMBE baada ya kumuomba mmewe yaani baba watoto wake pesa ya kununua sukari robo!

Tukio lilikuwa hivi, mme wa huyu mama alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kutenda kosa ambalo yeye mwenyewe alikili kuwa hakulitenda bali alisingiziwa!

Mwezi uliopita huyu bwana amemaliza kifungo chake na kurudi nyumbani kwake akiwa na afya njema, tatzo limekuja kujitokeza baada ya kufika nyumbani kwake mkewe alimtengea maji ya kuoga kama kawaida!

Baada ya kuoga tu akiwa amejipumzisha kitandani ndipo mkewe alipofungua mlango na kumkuta amejilaza kitandani huku akionekana kama mtu aliyekuwa na mawazo!

Ghafla mwanamke yule alimwambia mmewe" Baba Baraka naomba pesa nikanunue sukari robo, maharage robo!""

Yule bwana aliyetoka jela ghafla alijikuta ameishamtia mkewe ngumi ya chembe huku akimtaka amwambie kama jela wanagawaga pesa!

Mwanamke hata umwambie huna pesa yeye hawezi kukuamini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeangalia niko jukwaa gani kumbe ni la udaki ndruuki
 
Huu ndiyo mtaji wa CCM, umasikini wa wa-Tanzania
 
Back
Top Bottom