Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Mwanamume mmoja huko Kayole, Kenya anayetambulika kama Evans Kidero Okoth anauguza majeraha mabaya kichwani baada ya ugomvi mkali baina yake na muuza bar, anayetambulika kama Mary Angara.
Siku ya tukio, Bi Angara alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na alikuwa akiwakarimu vipande vya keki na chakula na wateja wake ndani ya baa hiyo. Kidero, ambaye alikuwa ameketi mwenywewe na vinywaji vyake kwa alikataa vyakula hivyo.
Kukataa kwake kulionekana kumuudhi sana Bi Angara, ambaye alimshtumu ghafla kwa kumdai KSh800.
Kidero kwa mshutuko alisisitiza kuwa hatalipa kiasi ambacho hajui. Ugomvi ulianza, na ghafla Bi Angara alikimbia hadi eneo la jiko la baa, akachukua sufuria ya kupikia na kumpiga Kidero kichwani mara mbili, na kupelekea kupoteza fahamu pale pale sakafuni.
Bwana Kidero alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta kwa matibabu zaidi.
Baadaye Angara alikamatwa na kufikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Makadara. Alikana kosa lolote na kwa sasa yuko nje kwa dhamana ya KSh10,000 pesa taslimu.
HASIRA HASARA!