SoC02 Aplikesheni mkombozi

SoC02 Aplikesheni mkombozi

Stories of Change - 2022 Competition

Morioh

New Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Stories of change; Aplikesheni mkombozi.

Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana wengi wa Kitanzania ni moja kati ya matatizo ambayo mpaka sasa halijaweza kutatuliwa kikamilifu. Sio tu Tanzania, bali tatizo hili ni tatizo ulimwenguni pote. Moja wapo ya sababu kuu kwanini vijana wengi hawapati ajira sio elimu, bali ni vyanzo vya ajira hizo.

Vijana wengi wenye elimu ya chuo kikuu yaani shahada, hawana ajira sio kwamba walimaliza elimu yao ya chuo kikuu vibaya hapana, ila ni kwasababu kila waendapo kutafuta ajira wanakosa au wanaambiwa hakuna nafasi za kazi au pengine hawaangalii mahala husika.

Je, nini kitatokea kama kutakua na aplikesheni ambayo itaweza kuwakutanisha waajiri na wenye haja ya ajira hizo? Sio kweli kwamba kila unachosoma chuo kikuu ndo ambacho utakua na ujuzi nacho pekee. Mtu anaweza kuwa amesomea shahada ya kitu kingine na akawa na ujuzi na icho alichosomea na maarifa mengine ya ziada na ya muhimu ambayo yanaweza kumpatia ajira. Kiuhalisia, watu wengi hawafanyii kazi shahada walizonazo, asilimia kubwa wanafanya kazi ambazo zina hitaji elimu kidogo waliopata wakiwa shuleni na kutumia maarifa yao ya ziada zaidi kuliko elimu yao!

Katika aplikesheni hii, itaweza kuwa inafikiwa na wanaotoa ajira na wenye kutaka ajira izo. Kwa upande wa waajiri watajaza nafasi za kazi zilizopo katika taasisi yao, sifa za mwombaji, maarifa wanayohitaji na mda wa mwisho wa kutuma maombi. Na wanaotafuta ajira hizo, watapaswa kutengeneza ‘profile’, ambapo watajaza taarifa zao binafsi kama vile umri, majina yao, wanapoishi na taarifa kuhusu elimu zao. Lakini pia watahitajika kujaza maarifa ya ziada yenye manufaa ambayo wako nayo.

Nitatoa mfano, mtu anaweza akawa na shahada ya sheria lakini akawa na maarifa kama vile ‘ Data analysis (Advanced excel, spss & stata)’ au akawa na maarifa ya graphic designs au mechanics. Mtu huyu anaweza akapata nafasi ya kuajiriwa katika taasisi yenye kuhitaji mtu anaweza kufanya Data analysis.

Ni kweli kuna tovuti za taasisi na mashirika mbalimbali ambapo ni katika tovuti hizi ndipo matangazo ya kazi kati taasisi husika huwekwa. Siku izi kumekuwa na utapeli mwingi mno, tovuti zenye taarifa za kizushi zimekua nyingi mno kiasi cha kwamba inakua vigumu sana kutambua ipi ni taarifa halali kwenye tovuti halali na ipi ni ya ubabaishi tu. Kwa karne hii ya sasa matumizi ya tovuti yamekua ni ya taabu kidogo ukilinganisha na matumizi ya aplikesheni husika. Ni rahisi sana kujisajili na kujaza taarifa zako kuliko kutembelea tovuti moja moja ama ofisi ukitafuta kazi. Katika karne hii vijana wametekwa matumizi ya mtandao yaani ‘social media’ kama ambavyo watu wanatangaza nafasi za kazi katika Instagram na facebook kwanini isitengenezwe aplikesheni ambayo itakua ni mahususi kabisa kwa ajili ga kutangaza nafasi za kazi tu?

Aplikesheni hii itatengenezwa kwa namna ambayo mtumiaji akishatengeneza ‘profile’ yake na kujaza taarifa zake anaweza akapata taarifa kama ‘notifications’ kwa kazi ambazo zitakua zimewekwa na taasisi mbali mbali ambazo zinaendana na sifa na maarifa aliyonayo mwombaji. Ni rahisi zaidi kama tukitumia aplikesheni kwa namna hii kuliko tovuti au kwenda katika maofisi husika.

Pia, taasisi zitakua na akaunti katika aplikesheni hii ambapo watakua wakieka nafasi za ajira zilizopo katika taasisi yao hii lakini pia wataweka fomu ya maombi ambayo itajazwa na wale wote ambao watakua wamepokea taarifa za nafasi za kazi kulanda na sifa na mahitaji yao. Yaani kama nafasi ya kazi iliyowekwa ina baadhi ya sifa na maarifa ya mtafutaji ata kama sio zote, basi mwombaji huyo atapata taarifa katika kifaa chake cha teknolojia chenye aplikesheni hii.

Tunafahamu kuwa aplikesheni au tovuti za namna hii zimekwisha kuwepo mfano linkedn na ajira portal. Tofauti ya hii ni kuwa itakuwa ina uwezo wa kusaidia mtu kupata taarifa pale ambapo kazi yenye uhitaji wa maarifa aliyonayo mtafutaji. Aplikesheni hii itatengenezwa kwa namna ambayo ‘alogarithm' yake itakua na uwezo wa kuoanisha sifa na maarifa ya mtafutaji na yale ya kampuni na moja kwa moja kumpatia mtafutaji taarifa iwapo mtu huyo atakua na ‘profile’ endapo baadhi ya sifa au maarifa yataoana.

Hii itakua ni aplikesheni ambayo kama vile tunavofungua akaunti za Instagram, twitter na facebook. Tofauti yake ni kuwa itakua kwa ajili ya kazi tu. Tumekua tukisikia kuwa ujasiriamali unaweza ukamkomboa mtu hata mwenye stashahada lakini ukweli ni kwamba mfumo wetu wa elimu Tanzania hautufundishi sisi kuwa wajasiriamali lakini pia hatuwezi sote kuwa wajasiriamali. Wengi wetu tumekua tukiamini kuwa “nitasoma nifaulu nipate kazi nzuri.” Ni lazima tukubaliane na suala kuwa akili zetu sio sawa na ujasiriamali sio kwa ajili ya mtu yoyote. Wapo wale ambao wanaweza kufanya vitu vingine ambavyo ni vya kitaaluma zaidi kama vipaji vyao.

Nafikiri ni wakati sasa Tanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla uwafikirie wale ambao wamekwenda shule na wakapata shahada zao lakini bado wanahangaika mitaani bila ajira yoyote ingawaje wana maarifa mengine zaidi yenye manufaa. Ninaamini kuwa kwa kuwasaidia vijana hao tutaweza kuukuza uchumi wa Tanzania yetu kwa asilimia kubwa sana na kuleta maendeleo nchini kwetu. Nina imani kubwa kabisa kuwa aplikesheni hii itasaidia watu wengi sana wenye shida ya ajira.

Author; El. Morioh.
 
Upvote 1

Mimi naitwa Lumola Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Back
Top Bottom