App ya HIV Test kwenye simu inatoa majibu yaliyo sahihi?

oluku

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
350
Reaction score
71
Majuzi katika mitandao ya jamii nimetumiwa app ya HIV test inayotaka kudownload kwenye playstore ambapo ukishadownload unaweka kidole kwa muda kama Dk 1 ina scan inakupa jibu kama una virus au hauna.

Swali langu ni Je, App hii ina ukweli wowote katika majibu yake maana haiko consistent!?

Naamini huku kuna wataalam wa afya wanaoweza kutuambia iwapo wanaijua hii app na ufanisi wake.
 
Ngoja waje maana hata Mimi nilikuwa najiuliza sana juu ya hilo swala
 
Sure...kuna jamaa alifanya utani afu ikamwambia anayo du ikabidi nimtulize kuwa si ya kweli
 
Ndugu yangu usidanganyike. Virusi viko kwenye damu. Huwezi kuvipima kutumia ngozi ya kidole
 
Ngoja waje maana hata Mimi nilikuwa najiuliza sana juu ya hilo swala

hivi mtaanzaje kufuatilia hizo apps... kwa vyovyote vile hizo ni games tu...
uki-download ni sawa na kupoteza mb bure.

si za kweli achaneni nazo.
 
hivi mtaanzaje kufuatilia hizo apps... kwa vyovyote vile hizo ni games tu...
uki-download ni sawa na kupoteza mb bure.

si za kweli achaneni nazo.

Sasa kwanini wanaziweka?, je wanataka tu waibie watu?, kama hivyo kwanini serikali inaacha hali hiyo iendelee?
 
Sasa kwanini wanaziweka?, je wanataka tu waibie watu?, kama hivyo kwanini serikali inaacha hali hiyo iendelee?

mkuu nishasema hizo ni games tu za kujifurahisha. Serikali kamwe haitazuia hicho, ni sawa na zile apps za kutrack caller location nyingi ni fake(just games) zinawekwa tu for funny...
 
Inawezekana ikawa na ukweli flani maana ipo ya kupimia haemoglobin na inatoa majibu, research ilifanyika juzi juzi Mwezi wa sita Muhimbili. Jamaa anatoka india
 
Inawezekana ikawa na ukweli flani maana ipo ya kupimia haemoglobin na inatoa majibu, research ilifanyika juzi juzi Mwezi wa sita Muhimbili. Jamaa anatoka india

Naomba link ya results za hiyo research au jina la huyo mtafiti toka India ili nijifunze namna inavyofanya kazi hiyo non-invasive technique.
 
Naomba link ya results za hiyo research au jina la huyo mtafiti toka India ili nijifunze namna inavyofanya kazi hiyo non-invasive technique.

Sawa ngoja nii Google na wewe pia unaweza kuigoogle. nikiipata naitupia hapa ila Nakumbuka kama vile alikua akiitwa Dr. Shah
 
Je wewe kwako imedetect positive or negative?
 
Be careful guys,not everything comes from europe is useful, especially matter concerning health issues.
 
Naomba link ya results za hiyo research au jina la huyo mtafiti toka India ili nijifunze namna inavyofanya kazi hiyo non-invasive technique.

Results za Muhimbili sina ila alikuja na aliletwa na shirika fulani kwajili ya kufanya hio kitu ili iweze kutumika kwenye mmojawapo ya miradi ya NGO hio.

Anaitwa Dr. Zahid Shah na hio app inapatikana kwenye Google playstore. Ipo App ya namna hio pia ambayo inapatikana kwenye Apple ila inauzwa. Kwahio kuna uwezekano hata hio ya HIV testing ikaja kuwa ya kweli
 
mkuu nishasema hizo ni games tu za kujifurahisha. Serikali kamwe haitazuia hicho, ni sawa na zile apps za kutrack caller location nyingi ni fake(just games) zinawekwa tu for funny...

Sasa viongozi wetu hawa Akina Mulogo,Muongo,Majimarefu na wenzao kweli jamani wazuie apps? Kwanza wanajua kuna apps fake duniani? Kwanza watakuuliza "apps ndio nani?"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…