App ya HIV Test kwenye simu inatoa majibu yaliyo sahihi?

Malaria tu haipimwi kwa kuweka kidole kwenye screen ya simu sembuse ngwengwe!? Unacheza makida weye.
 
Hakuna hicho kitu duniani. Ni lazima upimwe moja ya blood fluids "Damu, Oral fluid (siyo mate) na mkojo" kutoka katika mwili wako.

 
tusijidanganye kwa vipimo ivi nenda hosp ukacheki kwa uhakika zaidi
 

"Njia pekee ya kukomesha HIV/AIDS ni kuacha/kukataa kupima HIV".Bado kuna wajinga wengi sana kwenye nchi za dunia ya tatu ambao bado hawajui kwamba hakuna AIDS inayosababishwa na HIV.ARVs ndio sababu halisi ya vifo VYOTE vinavyowatokea wale wanaozitumia.

Ukiweza kuitumia akili yako vyema katika kuhoji na kudadisi kuhusu HIV/AIDS,huo ndio utakuwa ukombozi wako kifikra kuhusu HIV/AIDS,na hapo ndipo utakapojua kwamba "HIV/AIDS IS JUST MINDSET DISEASE".
 

Kivipi embu fafanua. Kidogo
 
Kivipi embu fafanua. Kidogo

Hongera sana kwa kuuliza,kuuliza kwako ndio ukombozi wako kifikra;

Uongo kuhusu HIV/AIDS umelalia katika masuala makuu manne(4):

1.Historia yake ni uongo mtupu,
2.Nadharia yake (kwamba HIV husababisha AIDS na HIV/AIDS huambukizwa kwa njia ya ngono,na kwamba AIDS haina dawa) ni uongo mtupu,
3.Vipimo vya 'HIV' ni kanya boya,yaani vya uongo/feki/vya kitapeli,havipimi kijidudu chochote,
4.Vidonge vya ARVs havina faida YOYOTE ile zaidi ya hasara,na ndio hivi vidonge vinavyosababisha AIDS ya ukweli kwa wale wanaovitumia.ARVs husababisha Cancer,matatizo ya ini,figo,moyo,kisukari,upungufu wa damu nk ambayo ndio matatizo yanayowaua wale wanaozitumia.

Si rahisi kujua ukweli huu kwa sababu zifuatazo;

1.Unahitaji kuwa na uelewa kuhusu baiolojia na kemia ili ikusaidie kudadavua,
2.Unahitaji kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu historia ya serikali ya Marekani kuanzia mwaka 1910,
3.Unahitaji kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu siasa za kimataifa,
4.Unahitaji kuwa na uelewa kuhusu uhusiano wa mwanadamu na mazingira yake,
5.Unahitaji kuwa mdadisi sana,mwepesi kuelewa mambo mapya na kutumia mantiki/logic katika kudadisi,
6.Unahitaji kuwa tayari kupokea mambo tofauti kabisa na jinsi uyaelewavyo sasa.

Watu wengi hawana sifa hizi,ndio maana wengi wanaishi kama mifugo na kupelekwa kokote kulingana na matakwa ya mchungaji.Na ndio maana hautakuja kusikia inatangazwa kwamba dawa ya HIV/AIDS imepatikana,hii ni kwa sababu hakuna ugonjwa kama huu,hivyo huwezi kupata dawa ya ugonjwa HEWA.

Kwa kukusaidia zaidi pitia uzi huu hapa chini kwa umakini mkubwa,huu ndio msaada wangu kwako, hata nikifa leo utanikumbuka kwa hili;

https://www.jamiiforums.com/jf-doct...ye-ukimwi-tena-peku-na-asipate-ukimwi-64.html
 
Kuna kipimo kingine kinaitwa quantum magnetic Resonant.hasa wanakitumia Fore Plan Clinic ya dr Mwaka mbona hawapimi damu na wanagundua magonjwa mengi?.hapa ningependa dr mwenye maujuzi atueleze
 
Hospitali wanapima bure. Sa wewe badala ya kwenda Hospitali kupima unahangaika na application za simu, endelea tu kupima iko siku utapata matokeo ya unachokitafuta
 
Niliwahi kuweka moja kwenye simu yangu, unagandamiza kidole baada kama test ya kwanza, baada ya hapo inafuata test ya pili ambayo unaulizwa maswali kama kuhusu unavyojihisi/kujisikia mwilini, kwa mfano inakuuliza kama unahisi maumivu kwenye viungo vya mwili, ngozi kupauka, kupungua uzito, kichwa kuuma nk halafu mwishoni inakupa majibu kwa namna ya "possible" kulingana na dalili za mwili wako zilivyoonesha, kwahiyo utaambiwa kuwa una uwezekano kuwa una vvu kwa asilimia 80,90 nk au kuambiwa kuwa kuna uwezekano wa asilimia hizo kuwa hujaambukizwa au upo kwenye hatari ya kupata maambukizi. Sikuona jibu la moja kwa moja kuwa ni positive au negative.

Nilichogundua ni kuwa app inafanya kazi kama daktari tu anavyochukua maelezo yako na kisha kuhisi tatizo linalokusumbua, hivyo naamini kuwa hizo apps haziwezi kupima HIV/AIDS kwa kuwa VVU wapo kwenye damu, au labda kuna apps zinazopima kwa kuhusisha screen ya simu na damu.
 
Kuna kipimo kingine kinaitwa quantum magnetic Resonant.hasa wanakitumia Fore Plan Clinic ya dr Mwaka mbona hawapimi damu na wanagundua magonjwa mengi?.hapa ningependa dr mwenye maujuzi atueleze

hao wanatumia miisho/ncha za neva zilizo kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu.
wanatambua kama kiungo fulani mwilini hakifanyi kazi vizuri lakini hawawezi kupima magonjwa kama typhoid, AIDS au amoeba kwa hiyo njia.
 

Attachments

  • 1443687886199.jpg
    9.9 KB · Views: 242
hao wanatumia miisho/ncha za neva zilizo kwenye viganja vya mikono na nyayo za miguu.
wanatambua kama kiungo fulani mwilini hakifanyi kazi vizuri lakini hawawezi kupima magonjwa kama typhoid, AIDS au amoeba kwa hiyo njia.

Je wanaweza pima kisukari kwa njia hii?
 
Duh! Hili Jukwaa Lina Wagonjwa Wengi Aisee! Na Magonjwa Pia Yatakuwa Mengi Humu, Ngoja Nirudi Kule Kwangu Siasani! Nikikaa Sana Huku Naweza Rudi Na Ugonjwa Kule Jukwaa La Siasa! Jioni Njema Wagonjwa!.
 
hizo no biashara tu watu wanatengeneza app ili biashara iende.ni kama app ya blood group ukiweka kidole Mara itakuonyesha group B + ujijaribu tena itakuletea group o.hazina ukweli wowote bila ya kupima damu
 
Je wanaweza pima kisukari kwa njia hii?

hapana...ila kwa kuangalia tu viashiria mbalimbali anaweza akajua kuwa huenda mtu ana kisukari, ila kuna kupimo maalumu cha kisukari kisichohitaji damu.
 
hapana...ila kwa kuangalia tu viashiria mbalimbali anaweza akajua kuwa huenda mtu ana kisukari, ila kuna kupimo maalumu cha kisukari kisichohitaji damu.

Kinaitwaje na kinapatikanaje? Tafadhali nijuze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…