Mimi nasimana upande wa Kikuu.
Kumbuka kuwa Hawa watu wanaendesha biashara yao kupitia mtandao, na bidhaa zao wanazouza zinatoka moja kwa moja nchini China.
Ukiagiza bidhaa, unapewa time line ya kukufikia ni angalau wiki mbili, lakini inategemeana na wewe ulipo.
Hawa jamaa Wana mawakala wao ambao wako kila wilaya Hapa nchini na lengo lao ni kukufikishia mzigo wako mkononi Tena ukiwa katika ubora Kama jinsi ulivyouagiza.
Mimi hapa ni shuhuda wa Hawa Kikuu, kwani nilishaanunua saa mpya kutoka kwao na mpaka muda huu ninayo na inatumika.
Mzigo niliuagiza ndani ya siku 14 + 5 tu tayari niliitoa mkononi Tena kwa kuletewa na wakala ninapoishi.Siku 14 kutoka China mpaka Dar na siku 5 kufika mkoa nnapoishi.
Mzigo unaagizwa kupitia mtandaoni na unapewa Tracking number ili kuutazama ulipofika, na hii Tracking number inafanya kazi na unapokea mrejesho kila sehemu,mzigo unapofika.
Bidhaa zote zinatoka China,hakuna bidhaa inayotoka hapa Tanzania, kwahiyo uvumilivu wako tu ndo Jambo la msingi.