App zinazotoa mikopo mitandaoni zina riba kubwa sana, ukichelewa rejesho wanatuma SMS kwa namba zote ulizowasiliana nazo

Daaaaa hawa wapumbavu Pesamloan jana wamenitumia sms kuna mpuuzi kakopa huko wanamdai. Wanapataje namba zetu ndio swali?
 
Wanaedit picha zako wanatengeneza video ya ngono wanatuma kwa contacts zako zote
Wahindi wanajiua mno
Unapigwa miti vibaya kwenye hyo video uwe me uwe ke
Wanafanya hivyo ukishindwa kuwalipa au ukichelewesha marejesho?
 
mkopo wa kwanza wanaweza kukopesha kiasi gani.... nataka nijaribu kupata mzigo wa kutosha... wasijekua kama branch unaanza na elfu 5
 
Saa 6 unasikia tiruuuuuu.......Ka mlio ka meseji unaenda kuangalia unakutana na hii;

NDG........TUNAKUOMBA ULIPE DENI LAKO ULILOKOPA TAREHE........UNAJIFANYA MJANJA KUTUKWEPA LAKINI TUNAKUHAKIKISHIA HIVI SASA HUNA PA KUKIMBILIA MAANA TUMEKODI MAKOMANDO 13 KUTOKA CUBA NA ISRAEL WATAKAOKUSAKA KILA KONA, TUMEKODI WADUNGUAJI 6 KUTOKA SOMALIA, TUNAO MANINJA 11 KUTOKA JAPAN NA KIKOSI KAZI CHA WANAJESHI 9 WANAMAJI KUTOKA NAVY SEAL MAREKANI, URUSI IMETUPA WANAJESHI WANNE KIKOSI CHA ANGA NA VIETNAM IMETOA BATALION 2 JESHI LA ASKARI WA MIGUU

NB; LIPA HELA YETU BOYA WEWE
 
NARUDIA iwe PESA ONE, XPESA, SIJUWI UJINGA GANI.
MSIJARIBU, MTAJUTA.....
Kwanza hupewi hela utakayo! Tuseme umeomba 100,000/-, kwanza wanakata hiyo laki unatumiwa 50 au 55! Kisingizio sijuwi administration cost!
Lakini utatakiwa kulipa laki na riba juu!
UTAPELI WA KUFA MTU!
TUNAWAONYA WANA JF, MSIJARIBU KUSHUSHA HIZO APP NA KUOMBA MKOPO
 
Utaita maji mma
 
Woiiiii
Nimecheka sanaaa

Mdogo angu kakopa huko, wamedukua namba ya mume wake wakatuma msg ya kumdai pesa

Shemeji anataka kujua pesa imeenda wapi na kwanini dogo kakopa bila kumtaarifu

Aisee hizi application za kuzikimbia ntakomaa na MGODI tu wa vodacom
 
Wanaedit picha zako wanatengeneza video ya ngono wanatuma kwa contacts zako zote
Wahindi wanajiua mno
Unapigwa miti vibaya kwenye hyo video uwe me uwe ke
Duuuh! kwakweli wanakosea kama ni hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…