BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Apple imetoa mfumo mpya wa iOS 16.0.2 kwa watumiaji wa iPhone 8 mpaka iPhone 14 zote; ili kurekebisha matatizo ya Kamera za iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max.
Siku chache zilizopita baadhi ya watumiaji walikuwa wanalalamika kamera ya iPhone 14 Pro ilikuwa inatikisika na kutoa kelele kwa ndani. Matatizo hayo yalikuwa yanatokea pale mtu akitaka kurekodi picha au video kwa kutumia app za Snapchat, Instagram na TikTok.
Apple imefix matatizo hayo na imesisitiza watumiaji wote wa iPhone 14 kuweka update hii ili kusaidia Stabilizer ya kamera ya iPhone isiharibike.
𝗠𝗮𝘁𝗮𝘁𝗶𝘇𝗼 𝗺𝗲𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘆𝗼 𝘆𝗮𝗺𝗲𝗿𝗲𝗸𝗲𝗯𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝘀𝗶𝗺𝘂 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶𝗻𝗲 𝗮𝗺𝗯𝗮𝘇𝗼 𝘀𝗶𝗼 𝗶𝗣𝗵𝗼𝗻𝗲 𝟭𝟰:
1️⃣ Simu kuonyesha rangi nyeusi kwa muda mrefu; baada ya kufungua simu kwa mara ya kwanza
2️⃣ Ujumbe wa Copy and Paste ulikuwa unajitoa kabla mtu hajafanya maamuzi
3️⃣ Kuna baadhi ya iPhone 14 zilikuwa hazitoi mlio baada ya kuwasha simu