Mkuu umemiliki Samsung siku nyingi sana ndomana hujui jamaa kama wamechange, na kuhusu ubora wa kioo unawakosea sana Samsung maana Kwa android hakuna anaemzidi ubora wa kioo Samsung
Inaonekana we una judge ubora kioo Cha oppo toleo la sasa dhidi ya galaxy s 10 ya miaka hiyo, ila kinachonishangaza ni kutoka Samsung na kwenda Tecno na kuridhika na Yale mavioo Yao ya kupauka na ukaridhika na kuongeza tena tecno lingine ni wazi ulichelewa sana kujua simu nzuri ndugu yangu
Kuhusu charge pia Bado unaongelea Samsung za zamani, haya matoleo Yote ya A,M note series Yana battery iliyo vizuri sana, siku hizi ata watumiaji wa simu za Samsung unakuta wanapeta na battery yenye 5000mph
Samsung waligundua wanapoteza wateja wengi wa simu Kwakuwa simu zao ni ghari sana na wana tatizo la charge, kuanzia hapo wakatwist wakaleta simu za bei Chee na kuongeza ubora wa battery, kuhusu kioo hao ndio wanaongoza, kuhusu camera ni simu chache sana zinaikimbiza Samsung inategemea unalinganisha simu zipi
Unachotakiwa kujua ni kwamba Samsung wanakupa simu kulingana na mfuko wako, ndomana me pia napenda Xiaomi na oppo maana Hawa wanakupa ubora Mzuri kwenye pesa kidogo