Tetesi toka kwa Ming-Chi Kuwa kuanzia 2023 Apple ataanza kutumia USB type C.
Inawezekana ikawa ni shinikizo toka jumuiya ya Ulaya ikitaka makampuni yote ya simu yatumie standard moja ya kucharge.
Inawezekana ikawa ni shinikizo toka jumuiya ya Ulaya ikitaka makampuni yote ya simu yatumie standard moja ya kucharge.
- Tunachokijua
- Umoja wa Ulaya umelazimisha charge za USB -C kwa makampuni yote ya utengenezaji wa simu ikiwemo kampuni kubwa ya APPLE. Ambapo wanaharakati wa Jumuiya ya Ulaya (EU) wamekuwa wakifanya kampeni kwa zaidi ya muongo mmoja kwa ajili ya kutumia aina moja ya chaja, ili kuepuka uchafuzi wa mazingira unaotokana na kutupa chaja zilizoharibika.
Watu wengi huweza kumilika ziadi ya chaja ya aina moja na hivyo kupelekea kuongezeka kwa vifaa vya kielekroniki majumbani jambo linalofanya kuzidi kuongezeka kwa takataka. Kwa kutumia chaja ya aina moja TYPE-C itasaidia gharama na pia kupunguza takataka zinazokadiriwa kufikia hadi tani 11,000 ndani ya mwaka.
Awali, kampuni ya Apple waligoma kutumia TYPE-C kwa kigezo kwamba itazuia ubunifu wa teknolojia. Lakini, katika toleo la simu la iPhone 15, kampuni hii itaanza rasmi kutumia utaratibu wa kuchaji kwa kutumia USB-C kama ambayo Bunge la Ulaya limetaka.
Kampuni ya Nokia, Samsung na wengine wa Android walikubaliana na hilo na wameanza kulifanyia kazi. Ambao Umoja wa Ulaya unadai kuwa ifikapo 2024 Makampuni hayo yaweze kuzalisha chaja za TYPE-C kwa ajili ya matumizi ya simu zake.
Kwa mujibu wa taarifa Rasmi ya Bunge la Umoja wa Ulaya, Mpango huu unapaswa kutekelezwa na makampuni yote ya simu ifikiapo mwishoni mwa mwaka 2024.
Aidha, masharti haya yataongezwa kwenye vifaa vingine kama laptops ifikiapo mwaka 2026. Kwa muktadha huu, watumiaji wa vifaa hivi hawatapaswa kutumia chaja tofauti kila wanaponunua kifaa kipya.