Apple waja na iphone ya bei nafuu iphone SE (2020)

Apple waja na iphone ya bei nafuu iphone SE (2020)

Samsung, huwaei na oneplus wamewakalia pabaya wazee wa apple hata ubunifu umeisha kabisa, simu hiyo ni basic sana kwa huu mzigo wa pesa.
atleast sasa tuwasifie kwa kuamua kuiga wengine wanachofanya.huwezi ukajidai miaka yote kwamba wewe ni mzee wa premium products tu, hutoi za makapuku.

wenzie wana masimu kibao, mengine yanakaa charge sio kawaida, yeye akomae na ujinga hajipendi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu tupe uchambuzi bas

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwenye simu kitu muhimu kabisa ni soc, hii ndio inadetermine vitu kama
1. Nguvu ya processor
2. Uwezo wa Graphics
3. Speed ya internet
4. Uwezo wa Wifi
5. Uwezo wa bluetooth
6. Ukaaji chaji
7. Speed ya storage
8. Aina za ram etc

Sababu soc ya iphone se 2020 ni A13 inamaana mambo mengi hapo juu itakuwa nzuri kushinda A11 ya x,

Sema display ya x ilikuwa nzuri sana, kama wewe sio mdau wa App na magame mazito na matumizi ya kawaida X ni simu nzuri bado.
 
Wanaolalamika kuhusu chaji ni wale wanaishi kwa shemeji I can’t imagine siku nyingine mtu unakuwa busy hata kupokea Simu ama kujibu sms mtu unashindwa halafu uje uniambie berti ni ndogo sana


Sent using IPhone X
kuna mwingine biashara zake zinategemea simu kuanzia social networks mpaka kuwasiliana na wateja mara kwa mara.
 
laki nane sibora nikaanguka na fupa la A71 hata kwa kuongeza pesa kidogo? laki nane kabetri ka ujazo huo na hako kascreen waakti kuna akina one+ huko unapata unachotaka?
OnePlus huwezi kupata kwa laki nane labda toleo la miaka mitano iliyopita
 
kuna mwingine biashara zake zinategemea simu kuanzia social networks mpaka kuwasiliana na wateja mara kwa mara.

Biashara gani mkuu ya umbea kushinda Instagram masaa 12?kwahiyo utakuwa online unamsubiria mteja?


Sent using IPhone X
 
Biashara gani mkuu ya umbea kushinda Instagram masaa 12?kwahiyo utakuwa online unamsubiria mteja?


Sent using IPhone X
Mkuu nyingi mno, mfano online freelancer kwenye mtandao kama upwork inakulazimu muda mwingi uwe mtandaoni.
 
Wanaolalamika kuhusu chaji ni wale wanaishi kwa shemeji I can’t imagine siku nyingine mtu unakuwa busy hata kupokea Simu ama kujibu sms mtu unashindwa halafu uje uniambie berti ni ndogo sana


Sent using IPhone X
Kama hayo ndio maisha yako upo busy hadi unashindwa kupokea simu why utoe milioni kununua simu?
 
Mkuu ukitoa hiyo soc vitu vingine vyote ni kawaida sana sana!! $399 kwa muundo huo wa simu yenye LCD ni wizi!

Pia hata design ni poor!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa simu za 2020 even zile budget flagship za kichina zinacost hela nyingi, mfano oneplus ya bei rahisi zaidi ni $699 mwaka huu, hata K30 pro ni $425, hivyo hii simu ni rahisi kushinda Budget flagship za Kichina.

Hivyo mkuu japo unadowngrade display na battery life ila unapata mambo mengine mazuri zaidi.

Kwa fans wa ios inawafaa hasa dada zetu huku waache kupigwa refurb za iphone 7/8/xr/x/xs
 
Back
Top Bottom