Apple yaifungulia mashtaka kampuni inayomiliki Pegasus

Apple yaifungulia mashtaka kampuni inayomiliki Pegasus

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Kampuni ya Apple imeifungulia mashtaka kampuni ya nchini Israel ya NSO iliyotengeneza programu ya Pegasus kwa madai ya kuathiri watumiaji wa vifaa na huduma zake.

Mashtaka ya Apple dhidi ya NSO yanakuja wakati kampuni hiyo ikikabiliwa na msukosuko wa madai kuwa maelfu ya wanaharakati, waandishi wa habari na wanasiasa walikuwa walengwa wa programu ya upelelezi inayomilikiwa na kampuni hiyo.

Apple inalenga kuepusha kuingiliwa kwa faragha za watumiaji wake, ikitaka kuipiga marufuku ya kudumu kampuni hiyo kutumia huduma na vifaa vyote vya Apple.

Kufuatia ripoti za programu ya Pegasus kuweza kutumika katika vifaa vya kidigitali bila kusubiri kuruhusiwa na mtumiaji kwa kubonyeza kiungo (zero click), Apple ilitoa sasisho katika mfumo wa vifaa vyake mwezi Septemba kuondoa uwezekano wa kuruhusu programu hiyo kuingia katika vifaa vyake.

Mamlaka nchini Marekani imepiga marufuku ushirikiano wowote kati ya makampuni ya Marekani na kampuni ya NSO kwa madai kuwa kampuni hiyo iliwezesha ‘serikali za kigeni’ kufanya ukandamizaji.


f29380737f724ae2ef72999f805b8502
 
Apple kashikwa pabaya sana naona anatafuta hata katundu kadogo aingize walau uso wake tu kukwepa aibu.

N'way waboreshe ulinzi na pia napenda vifaa vyao kwa ajili ya kazi zangu tu naona hawana mpinzani, congole kwao.

20211124_125656.jpg
 
Back
Top Bottom