Ndio Ninachosema.
Ni kweli wana vibali lakini kuna ufake ndani yake ili kuizunguka serikali na kujificha.
Kampuni zingine zina app zaidi ya 10. Niliona sms zile za matangazo. SMS moja imemaliza kwa kutaja app zake.
Siku moja nilishangaa kupigiwa simu na namba moja ambayo niliwasiliana nayo back days kuhusu deni la app fulani. Siku hiyo napigiwa kuhusu kukumbushwa kulipa mkopo kwenye app nyingine. The same number.
Wahudumu kila siku wanabadilishiwa simu za kupigia wateja.
Wakiharibu sana wanabadili jina la app. Mfano M loan sasa wameibadili na kujiita Swift money, hawa ndio baba wa kudhalilisha wateja pamoja na app zingine zinazomilikiwa na kampuni moja.
Ndio kampuni yenye mtaji mkubwa, wanakopesha mpaka milioni 3 kwa app moja ukiwa mteja wao uliyelipa kwa mda wanaoutaka wao.
Ila riba zao ni haramu , 50% ulipe kwa siku 5 ni kweli?
Laki 5 unajikuta unalipa laki 7 na nusu.
Hii mikopo naijua vizuri, walishawahi kuniharibia kisa 56, niliumia sana. Ile app nikawalipa nikawasiliana na boss wao Mkenya wakanikopesha kama milioni 2 na ushehe sijawalipa mpaka kesho.