Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Naomba kwa kuuliza maswali haya:
Hivi Mtanzani wa kawaida unaweza kuendesha biashara ambayo haina vibali vya serikali huku ukitumia mitandao ya simu kufanya biashara na serikali ikashindwa kukubaini/kukukamata?
Tuchukulie imeshindwa kukukukamata, je serikali itashindwa hata kutoa agizo kwa makampuni ya simu kusitisha mara moja kufanya biashara na kampuni zako(kutoa mikopo na kupokea marejesho ya mikopo kwa kutumia huduma za Mpesa, tigopesa, Airtel Money, n,k)?
Je, haiwezekani hii ni biashara ya vigogo kukusanya fedha za kampeni kuelekea uchaguzi wa 2025 au kujitajirisha?
Kwa riba ya asilimia 35 mpaka 40 kwa muda wa siku 5 mpaka 6, haya makampuni si yanatengeneza faida kubwa sana?
Katika watanzania milioni 60, kama watanzania milioni 10 au 20 wanakopa kila siku na kurudisha hizo riba kubwa ndani ya siku 5 mpaka 6, si ni wazi hawa jamaa wanatengeneza mamilino kwa mwezi tena pasipo kulipa kodi?
Wangekuwa wanapata hasara, makampuni haya yangeendelea kuongezeka?
Umewahi kujiuliza jeuri ya haya makampuni kudhalilisha watanzania wanaipata wapi?
Ni kweli serikali na taasisi zake zote wameshindwa kudhibiti makampuni yanayotoa mikopo mitandaoni kwa riba kubwa na pasipo kuwa na vibali?
Bishara kama hizi zingefanyika huko Somalia wala tusingeshangaa lakini sio kwa nchi yenye serikali na yenye vyombo vya dola!!!
No wonder watu wanamiliki vilabu vya mpira na wengine kununua boda boda na kuzigawa kama njugu.