TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Salaamu members wote wa JF.
Leo ninatoa heko kwa kazi kubwa wanayoifanya moderators na pia natoa ushauri wa namna bora ya kuifaidi JF.
Sote tunajua sekeseke la mitandaoni kipindi hiki. Ni kipindi cha tahadhari lakini ni kipindi pia cha kuwavua fisi wote waliojivika ngozi ya kondoo. Siyo kazi ndogo hiyo.
Ni katika kipindi hiki pia moderators wetu wa JF wamekumbana na wimbi la hatari kabisa kutoka kwa wabaya katika kulinda uwepo wa JF. Wabaya wanalengo la kuizamisha JF yaani ipotee mitandaoni. Ni wabaya hawa wanadiriki ama kuanzisha uzi ama kuweka bandiko hapa JF ambavyo vinakinzana na ama na sheria zetu zinazotuongoza hapa JF ama sheria zetu za nchi ya Tanzania.
Umahiri wa moderators umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wabaya hawa kwa ama kuziondoa bandiko na nyuzi za kuhatarisha usalama wa JF ama kuwalima " ban" na kufuta nyuzi na mabandiko yao kwa pamoja. Kwa hili nawapa heko moderators na nawapa pole kwani kuna uwezekano mlilazimika kufanya kazi kwa muda mwingi wa ziada kupambana na wabaya hawa.
Siku za nyuma niliwahi kuandika humu JF kuwa mtu mwenye nia njema kabisa kabisa na uhai wa Taifa la Tanzania hawezi kuwaza kufanya njama za kuifuta JF. JF ni kiungo muhimu katika kutukutanisha jamii nzima ya Tanzania huku tukiheshimu miiko inayoongoza jamii yetu.
Kwa hiyo, ni jukumu letu "members" wa JF kuwasaidia kwa hali na mali moderators wetu wafanye kazi kwa ufanisi zaidi kwa sisi members kuweka nyuzi ama mabandiko yanayokidhi vigezo vya sheria za JF na sheria zetu za nchi. Pia twaweza kuwasaidia kwa kuwapa taarifa moderators wa uwepo wa ama uzi ama bandiko ambalo linavunja sheria za JF na sheria za nchi kwa kubonyeza kitufe cha "report" mara nyingi kinachokuwa chini kushoto mwa bandiko/ post.
Kwa mara nyingine, poleni na heko moderators wetu wa JF.
Ni mimi TUJITEGEMEE, Asanteni sana kwa kusoma bandiko langu na Mungu akubariki. Amina.