Appreciation: Poleni na Hongera sana JF Moderators

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Salaamu members wote wa JF.

Leo ninatoa heko kwa kazi kubwa wanayoifanya moderators na pia natoa ushauri wa namna bora ya kuifaidi JF.

Sote tunajua sekeseke la mitandaoni kipindi hiki. Ni kipindi cha tahadhari lakini ni kipindi pia cha kuwavua fisi wote waliojivika ngozi ya kondoo. Siyo kazi ndogo hiyo.

Ni katika kipindi hiki pia moderators wetu wa JF wamekumbana na wimbi la hatari kabisa kutoka kwa wabaya katika kulinda uwepo wa JF. Wabaya wanalengo la kuizamisha JF yaani ipotee mitandaoni. Ni wabaya hawa wanadiriki ama kuanzisha uzi ama kuweka bandiko hapa JF ambavyo vinakinzana na ama na sheria zetu zinazotuongoza hapa JF ama sheria zetu za nchi ya Tanzania.

Umahiri wa moderators umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wabaya hawa kwa ama kuziondoa bandiko na nyuzi za kuhatarisha usalama wa JF ama kuwalima " ban" na kufuta nyuzi na mabandiko yao kwa pamoja. Kwa hili nawapa heko moderators na nawapa pole kwani kuna uwezekano mlilazimika kufanya kazi kwa muda mwingi wa ziada kupambana na wabaya hawa.

Siku za nyuma niliwahi kuandika humu JF kuwa mtu mwenye nia njema kabisa kabisa na uhai wa Taifa la Tanzania hawezi kuwaza kufanya njama za kuifuta JF. JF ni kiungo muhimu katika kutukutanisha jamii nzima ya Tanzania huku tukiheshimu miiko inayoongoza jamii yetu.

Kwa hiyo, ni jukumu letu "members" wa JF kuwasaidia kwa hali na mali moderators wetu wafanye kazi kwa ufanisi zaidi kwa sisi members kuweka nyuzi ama mabandiko yanayokidhi vigezo vya sheria za JF na sheria zetu za nchi. Pia twaweza kuwasaidia kwa kuwapa taarifa moderators wa uwepo wa ama uzi ama bandiko ambalo linavunja sheria za JF na sheria za nchi kwa kubonyeza kitufe cha "report" mara nyingi kinachokuwa chini kushoto mwa bandiko/ post.

Kwa mara nyingine, poleni na heko moderators wetu wa JF.

Ni mimi TUJITEGEMEE, Asanteni sana kwa kusoma bandiko langu na Mungu akubariki. Amina.
 
Mbaya wa JF sio waanzisha mada bali serikali ya CCM yetu!! JF ikifungiwa au kufutwa sio kwa sababu ya waanzisha mada bali kwa sababu serikali yetu inataka kusikia yale tu inayopenda kusikia! Yale yanayoendelea Twitter yangekuwa yanamhusu Tundu Lissu au Mbowe, au hata Zitto Kabwe, na yakaletwa kwa nguvu ile ile hapa JF, ile mikwara inayotolewa hivi sasa wala tusingeisikia kwa sababu CCM na serikali yake ingependa tuendelee kuzisikia taarifa kama hizo! Lakini kwavile taarifa hizi ni za rais wetu, basi CCM na Dola katu hawatapenda kuzisikia!! Matokeo yake kinachoonekana ni kama "uzushi" unaweza kuwa halali endapo utatolewa dhidi ya watu wengine lakini itakuwa haramu dhidi ya viongozi wakuu wa nchi!!!
 
Ukweli hauwatendei haki Moderators wetu! Moderators wamefanya kazi kubwa bila kuonyesha upendeleo. Wanafuata sheria zote za hapa JF na za nchi bila kuangalia 'uso' wa Mleta uzi ama muweka bandiko!

Toka asubuhi ninakagua vyanzo vyangu vya habari sijapata hata kimoja kinachothibitisha kuwa Chama kinachoongoza serikali ya nchi hii, yaani CCM kwa makusudi kimewaamuru moderators kuruhusu mabandiko na Nyuzi za maoni kinayotaka. Mkuu kama una ushahidi huo, kwa heshima kubwa tupatie hapa hapa.

Moderators wanawashughulikia wanaoleta habari zinazokinzana na sheria nilizoeleza kwenye bandiko la kwanza la uzi huu!

Mkuu, hivi unafurahishwa kusoma mabandiko ama Nyuzi za kizushi, uongo, utapeli, kebehi, kejeli, lugha za kuudhi, kutishia usalama wa watanzania, na hata kutishia usalama wa uwepo wa JF mitandaoni!? Kwa rekodi nilizonazo mpaka sasa moderators wetu hapa wana chuja mabandiko na Nyuzi zenye muelekey wa tabia ovu nilizokuuliza hapo juu kama unafurahishwa nazo.

Mapungufu mengine yapo kwao lakini la kusimamia uwepo usiotiliwa shaka wa usalama wa JF moderators kwa sana wanastahili, kongole na heko na Hongera.

Asante.
 
Moderators wawashughulikia wanaoleta habari zinazokinzana na sheria nilizoeleza kwenye bandiko la kwanza la uzi huu!

Unfortunately; kwa wale wa siku nyingi, huko nyuma tulikuwa na moderators ambao walikuwa very objective lakini siku hizi naona kuna moderators MUBYAZI kawaleta wanaoelekea kama watu wa KITENGO vile.!

Nyuzi ambazo zinakosoa serikali/ccm kwa nia nzuri ndizo zinazohamishwa na kupotezwa!!! Hii inaipunguzia hadhi yake JF. Hao watu wa kitengo wameinfiltrate ili kupata identity ya members but I believe Mubyazi analilinda hilo.
 
Salaamu members wote wa JF.

Leo ninatoa heko kwa kazi kubwa wanayoifanya moderators na pia natoa ushauri wa namna bora ya kuifaidi JF.

Sote tunajua sekeseke la mitandaoni kipindi hiki. Ni kipindi cha tahadhari lakini ni kipindi pia cha kuwavua fisi wote waliojivika ngozi ya kondoo. Siyo kazi ndogo hiyo.

Ni katika kipindi hiki pia moderators wetu wa JF wamekumbana na wimbi la hatari kabisa kutoka kwa wabaya katika kulinda uwepo wa JF. Wabaya wanalengo la kuizamisha JF yaani ipotee mitandaoni. Ni wabaya hawa wanadiriki ama kuanzisha uzi ama kuweka bandiko hapa JF ambavyo vinakinzana na ama na sheria zetu zinazotuongoza hapa JF ama sheria zetu za nchi ya Tanzania.

Umahiri wa moderators umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwadhibiti wabaya hawa kwa ama kuziondoa bandiko na nyuzi za kuhatarisha usalama wa JF ama kuwalima " ban" na kufuta nyuzi na mabandiko yao kwa pamoja. Kwa hili nawapa heko moderators na nawapa pole kwani kuna uwezekano mlilazimika kufanya kazi kwa muda mwingi wa ziada kupambana na wabaya hawa.

Siku za nyuma niliwahi kuandika humu JF kuwa mtu mwenye nia njema kabisa kabisa na uhai wa Taifa la Tanzania hawezi kuwaza kufanya njama za kuifuta JF. JF ni kiungo muhimu katika kutukutanisha jamii nzima ya Tanzania huku tukiheshimu miiko inayoongoza jamii yetu.

Kwa hiyo, ni jukumu letu "members" wa JF kuwasaidia kwa hali na mali moderators wetu wafanye kazi kwa ufanisi zaidi kwa sisi members kuweka nyuzi ama mabandiko yanayokidhi vigezo vya sheria za JF na sheria zetu za nchi. Pia twaweza kuwasaidia kwa kuwapa taarifa moderators wa uwepo wa ama uzi ama bandiko ambalo linavunja sheria za JF na sheria za nchi kwa kubonyeza kitufe cha "report" mara nyingi kinachokuwa chini kushoto mwa bandiko/ post.

Kwa mara nyingine, poleni na heko moderators wetu wa JF.

Ni mimi TUJITEGEMEE, Asanteni sana kwa kusoma bandiko langu na Mungu akubariki. Amina.

Naunga mkono hoja mkuu.
 
Mabibi na mabwana Remmy Ongara aliwahi kuimba "kuwapa pongezi madereva wetu Tanzania."

Namtafuta Don Nalimison tuimbe wetu:

"Tuwape pongezi mods wetu JF."

Pameondokea wimbi la wapotoshaji lenye njama za kuwaaminisha wengine yao yasiyokuwapo.

Mifano ipo mingi. Palikuwa na uzi na kichwa potoshi hapa kuwa chadema waeleza sababu za kushiriki uchaguzi wa marudio Muhambwe. Uzi huo kwa hakika title na content ya uzi zilikuwa tofauti kabisa.

Uzi huo na mazaga zaga sasa umeunganishwa na kuweka kunakostahili. Heko sana mods kwa hilo.

Kuna hizi zingine zenye upotoshaji kama huo. Mara ooh fulani kama somo fulani hali title na contents ni tofauti.

Wanaofanya hivi si kuwa ni ajali bali wenyewe wanaita kuwa ni calculations yaani hila!

Upotoshaji na usipewe nafasi katika jamii iliyostaarabika.

Mods nyuzi zote ambazo title haziendani na maudhui ndani ya uzi, fyekelea mbali!

Hiiiiii.
 
Mabibi na mabwana Remmy Ongara aliwahi kuimba "kuwapa pongezi madereva wetu Tanzania."

Namtafuta Don Nalimison tuimbe wetu:

"Tuwape pongezi mods wetu JF."

Pameondokea wimbi la wapotoshaji lenye njama za kuwaaminisha wengine yao yasiyokuwapo.

Mifano ipo mingi. Palikuwa na uzi na kichwa potoshi hapa kuwa chadema waeleza sababu za kushiriki uchaguzi wa marudio Muhambwe. Uzi huo kwa hakika title na content ya uzi zilikuwa tofauti kabisa.

Uzi huo na mazaga zaga sasa umeunganishwa na kuweka kunakostahili. Heko sana mods kwa hilo.

Kuna hizi zingine zenye upotoshaji kama huo. Mara ooh fulani kama somo fulani hali title na contents ni tofauti.

Wanaofanya hivi si kuwa ni ajali bali wenyewe wanaita kuwa ni calculations yaani hila!

Upotoshaji na usipewe nafasi katika jamii iliyostaarabika.

Hiiiiii.
Kwenye huo wimbo wa kumshirikisha Don Nalimison , naomba na mimi niwepo! Nitaimba na kucharaza hii kitu 🎸 I am a Soldier🎶 I am soldier!!!!
 
Ni Kweli Heko kwao

Kuna watu walitaka walete Ukigogo na Uveronica huku Jf.
 
Back
Top Bottom