Hapa lazima watu wawajibike haraka sana kuanzia waziri, naibu wake, mkuu wa majeshi, mkuu wa base ya mbagala na askari wote wa kituo hicho. Inatia hasira kwa uzembe huu uliotokea na kugharimu maisha ya watu, mali zao nk. Hivi JK upo wapi? mbona hutangazi hali ya hatari?
Hatutaki kusikia eti mnaunda tume kuchunguza mlipuko huu zaidi ya kuwawajibisha wote waliohusika. Wadanganyika tumechoka na ubabaishaji! na tume zisizoisha. Mheshimiwa JK angalia au iga wakubwa wenzio wanavyo-act immeadiatealy pindi janga kubwa linapotokea.
Angalia mfanao wa swine flu ilipotokea tu UK, USA na kwingineko wakuu wa nchi hizo haraka sana walienda kwenye media na kuelimisha umma. Huu sio wakati wa akina Nchimbi kuongea kwenye media zaidi ya kujiuzulu na kutoa maelezo kwa wadanganyika.