APRM Tanzania na Namibia wakutana Zanzibar kuimarisha utawala bora

APRM Tanzania na Namibia wakutana Zanzibar kuimarisha utawala bora

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Watendaji wa Taasisi ya Mpango wa hiyari wa Kujitathmini katika vigezo vya utawala Bora wa Umoja wa Afrika (APRM) kutoka Tanzania na Namibia wamekutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman, katika mkutano uliofanyika ofisini kwake Mazizini, Zanzibar.
IMG-20241205-WA0054.jpg
Mkutano huo ulilenga kuimarisha utawala bora na kuendeleza uhusiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza katika mkutano huo, Mheshimiwa Waziri Haroun alielezea hali ya utawala bora Zanzibar, akiipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanashirikishwa moja kwa moja katika maamuzi ya Serikali.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Bw. Lamau Mpolo, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi hiyo ili kuhakikisha misingi ya utawala bora inaimarishwa na kuendelea kudumishwa.
IMG-20241205-WA0056.jpg
Naye Mtendaji Mkuu wa APRM Namibia, Balozi Lineekela Mboti, alibainisha kuwa Namibia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuimarisha uhusiano uliopo na kubadilishana uzoefu katika masuala ya utawala bora.

Mkutano huo umetajwa kuwa wa mafanikio, ukiweka msingi wa hatua zaidi za kuimarisha utawala bora katika nchi hizi mbili.
IMG-20241205-WA0058.jpg

IMG-20241205-WA0052.jpg
IMG-20241205-WA0050.jpg
 

Attachments

  • IMG-20241205-WA0048.jpg
    IMG-20241205-WA0048.jpg
    405.8 KB · Views: 2
Back
Top Bottom