Aqua Power Tanzania Limited yafungua kesi ICSID ikidai Tanzania fidia ya bilioni 1.3 kisa kunyanyaswa na kunyimwa leseni miradi ya nishati

Sijaweza kuona in details ila mbona claims zao ni ujinga? Yaani ukitaka leseni lazima upewe na ukinyimwa basi unadai fidia?

Kweli Tanzania tumeonekana mazombi na mapoyoyo kweli aisee, shamba la bibi watu wanajichotea tu

Na kwa miana sheria yetu utashangaa jamaa wanashinda hii kesi
 
Kampuni zilizosajiliwa Mauritius au zenye Branch huko Nyingi ni za kitapeli wale waliokubuhu.
 
Hawa ni watanzania wenzetu wanatupiga kwa mgongo wa makampuni ya kigeni ila ndio hivyo tumekosa kiongozi wa kuyasimamia haya.
Viongozi wa serikali hii chini ya CCM wana fursa ya kurekebisha mambo ili kuyafanya kuwa bora, lakini kwa hofu tu na woga wa kupoteza ulaji kupitia madaraka na mamlaka yao, wameshindwa na hawataki kuzitumia fursa hizi...!

Chanzo cha matatizo yetu haya yote yanaanzia kwenye udhaifu wa mfumo wetu wa kikatiba na kisheria. Lakini tukipata kiongozi anayeweza kuweka maslahi yake binafsi pembeni akakubali tufanye constitutional reforms, atakuwa ametatua robo tatu ya matatizo ya umasikini wetu na hivyo ujinga huu kupungua kama si kwisha kabisa...
 
Katiba na mambo ya utapeli wapi na wapi?
 
Wanaoandaa hii mikataba ni watanzania wenzetu wakishirikiana na wenye makampuni na kwa kuwa wanataka zile 10% basi huacha matobo ya kisheria ambayo husababisha nchi kushitakiwa makusudi na kushindwa kesi ili wapate pesa.
Na kesi hii wanakwenda kutushinda kwani walioandaa mkataba ndio watakaoiwakilisha serikali mahakamani na kujenga haja dhaifu!
 
Hivi hadi Leo hayo makampuni bado hayajui kwamba Tanzania ni nchi yenye utawala wenye itikadi ya Kikomunisti/ujamaa??

Wewe Beberu wacha Uwongo.

Tanzania haijawagi kuwa na Utawala ama itikadi ya Kikomunisti.

Ujamaa sio Ukomunisti.

Tanzania kama nchi zingine za Afrika na Amerika zilikataa kuingia kwenye vita baridi kwa kukataa kushoboke mifumo hiyo ya Ubepari na Ukomunisti.

Waliunda Non Aligned Movement kwanini?
Uzoefu kutoka duniani kote unaonyesha na kuthibitisha kwamba hakuna uwekezaji wa maana ambao unaweza kuwa economically viable kwenye nchi ambayo ina utawala wa kikomunisti,

ndio maana unaona hata raia matajiri wengi Sana kutoka nchi Kama Urusi au China wanazikimbia nchi zao na kwenda kuwekeza kwenye nchi zingine zisizokuwa na itikadi za ukomunisti.
Walipataje huo utajiri kama unasema huwezi kuendelea kama unafuata ukomunisti?
Wanafikiri matajiri hao ni wajinga??
Yawezekana sana tu ni wajinga. Unaacha nchi yako na wananchi wako kwenda kuwatajirisha wengine? Huo ndio mchango wake kwa Jamii? Kutelekeza watu waliomjenga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…