'
Aquarium' ni chombo cha kuhifadhi viumbe wa majini, ama wa maji baridi au ya chumvi, au ni kituo kinachotumika kuonyesha au kujifunza mkusanyiko wa viumbe wa majini.
Hutengenezwa kwa kioo ambacho hushikilia maji na hutumika kufugia na kuonesha wanyama na mimea ya majini. Huweza kuwa na ukubwa tofautitofauti kuanzia maumbo madogo ya mezani hadi vituo vikubwa vya umma.
Kumekuwepo na kipande cha video kinachosambazwa mtandaoni kikionesha inayodaiwa kuwa 'aquarium' kubwa imeporomoka huko California na kuua watu 50.
Kulingana na
Google Trends kipande hicho cha video kiliibua wimbi kubwa zaidi la watu kuongezeka kwenye Google siku ya Jumatano, wakati watumiaji walipotafuta kuthibitisha ukweli wa video hiyo.
Ufuatiliaji wa JamiiCheck
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search pamoja na utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa video hiyo si ya kweli, kwani halijaripotiwa tukio hilo na vyanzo rasmi au ripoti za mamlaka husika bali video imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba.
Yapo mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa Akili Unde ikiwemo, kupotea ghafla kwa sehemu ya viungo vya mwili kwa baadhi ya watu, Kutokuonekana kwa vioo vilivyovunjika, uwepo wa watu wanaoonekana kuangukia upande wa ndani baada kioo kudondoka, licha tukio hilo bado kuna watu wanaotembea uelekeo ambapo maji yanaporomoka jambo ambalo si la kawaida kwa matukio hatari kama hilo.