Smart codetz
JF-Expert Member
- Jan 25, 2023
- 218
- 875
Ndugu Wananchi kwa dhati ya moyo wangu niwapongeze kwa kufika uwanjani kutoka kona zote nchini, mliosafiri kwa anga, mliosafiri kwa magari, mliopanda Pikipiki, mliopanda boti hadi Watembea kwa miguu, yote ni kwa ajili ya Yanga Afrika, huu sio tu upendo bali mahaba ya kulevya kwa klabu hii bora zaidi nchini.
Ndugu Wananchi poleni mno kwa kadhia ya leo, sisi kama Viongozi mliotupa dhamana kusimamia hii chapa kwa niaba yenu tumepigana, tumehakikisha mawazo yenu, matakwa yenu na sauti yenu inasikika kwa sauti ya juu sana, kwa kuheshimu mpira wa miguu na kuheshimu uthubutu wenu tuliandaa na kuleta timu uwanjani tayari kwa kushindana ila yaliyotokea yametokea.
Ndugu Wananchi, poleni kwa kupoteza muda wenu, kwa kupoteza fedha zenu kwa ajili ya mechi hii kubwa na ya kihistoria, ninyi ni sisi na maumivu haya ni yetu sote kama ambavyo tumeimba pamoja, tumelia pamoja basi hata sasa mpaka milele tupo pamoja, hilo likae vyema kwenye kumbukumbu kuwa sisi ni Yanga.
WACHEZAJI na Benchi la Ufundi, asanteni kwa heshima mliowapa Wapenzi wa soka nchini bila kujali timu zao, mmehakikisha mpira wa miguu umeshinda, kuna wakati sio suala la Mshahara wala posho bali heshima kwa nembo ya Kijani na Njano, Asanteni Vijana kwa kufika na angalau Mashabiki wameweza kuwaona na kuwalaki.
WANANCHI, mechi yetu dhidi ya Mtani wetu SIMBA imeisha leo hii kwa msimu wa 2024/25 raundi ya pili na ieleweke vyema hakutakuwa na mechi nyingine sehemu nyingine, siku nyingine na tarehe nyingine yoyote ya kuihusu Yanga dhidi ya Simba kwa Ligi kuu, iwekwe sawa kwenye kumbukumbu na ikolezwe vyema kwa wino kuwa its done and dusted, sisi tunasonga mbele na ratiba zingine.
Hii ndio sauti yenu moja, kamba moja ya DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO na tutashikilia hapo hapo Wananchi, niwatakie safari njema Wananchi wote kurejea makwenu, Mungu awalinde, awatunze mkaungane tena na familia zenu, tutakutana tena wakati mwingine panapo majaaliwa In shaa Allah.