Ardhi inalia kisa chupa za plastiki

Ardhi inalia kisa chupa za plastiki

robbyr

Senior Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
129
Reaction score
221
IMG_20220418_132242_710.jpg

Picha: My Camera
"Hatuna dunia nyingine. Lazima tuitunze na kuihifadhi." – Wangari Maathai

Kuna mdau aliandika hapa kuwa mmeamua kupamba jiji la Dar kwa chupa za plastiki. Sasa hii hapa ni Kilimanjaro na ni picha ya eneo moja

Kama elimu yaijatukomboa fikra zetu basi hata sheria na kanuni zimeshindwa.

Huu uchafuzi unadhirisha kabisa athari ndogo ya maarifa yanayopatikana katika elimu yetu.

Ushauri: Serikali iweke sheria chupa ziuzwe gharama kidogo kama shilingi 100 au 70 kwa moja ili ziweze kurudi viwandani. Bakheresa na Mo wasiwaze faida tu na pia serikali isiwaze kodi tu kwani kwa madhara ya muda mrefu tutaumia sana.

Ndugu wananchi na sisi ni lini tutaacha uchafuuuu?
 
Serikali itoe ruzuku kwenye mashine za kusaga chupa kwa vijana kila mtaa kuwe na mashine wanunuzi wapo wengi wa taka za plastic zilizosagwa.
Pia itoe mafunzo kwa vijana wajiajiri kutengeneza bidhaa aina zaidi ya 200 zitokanazo na taka za plastic mfano taka za plastic zinazalisha
.petrol, diesel,tiles, pavers, roofing tiles,mbao, furniture,vigae vya chini na vya kuzeeka nyumba pia,mifagio ya ndani,matofali ya kujengea,kamba na nyuzi,madawati,viti,meza,stuli, panels za kujengea, barabara nk.
Kila changamoto ni fursa.
Kila uchafu ni malighafi za kuzalisha bidhaa zingine.
 
Hizi energy drinks uchwara hizi yani asilimia 70 ya chupa hapo ni energy drinks aisee
 
Very simple. Serikali ipige marufuku chupa za plastic za rangi. Iruhusu kama zile za maji tu.
Mbona soda take away zopo kwenye chupa clear za plastic?
Kwa kufanya hivyo hakuna chupa itazagaa,zote zitaokotwa kurudi kiwandani.
 
Back
Top Bottom