SoC04 Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo tunapaswa kuithamini na kuitunza kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo

SoC04 Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo tunapaswa kuithamini na kuitunza kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo

Tanzania Tuitakayo competition threads

nafkiri

New Member
Joined
May 6, 2024
Posts
2
Reaction score
0
THE STORY OF CHANGE
Kutokana na ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania bara kutoka milioni 33.5 sensa ya mwaka 2002 hadi milioni 44.92 sensa ya mwaka 2012, na kufikia milioni 59.851 sensa ya mwaka 2022, kumekuwa na ukuaji mkubwa wa miji na ongezeko la mahitaji ya ardhi kutokana na upatikanaji wa elimu na ubunifu katika njia za kujiajiri. Hali hii imeleta wimbi kubwa la matangazo ya viwanja vinavyouzwa barabarani, masokoni, vituo vya daladala na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu. Watu wameona fursa katika kuwekeza katika ardhi kwa kununua, kukata, na kupima viwanja kwa ajili ya mashamba na makazi. Hii ni dalili nzuri inayoonyesha ubunifu na uwezo wa kufikiri. Hata hivyo, kuna maswali ya msingi yanayopaswa kujibiwa:
  • Je, uuzaji huu wa ardhi unazingatia kanuni na sheria za ardhi?
  • Je, upimaji wa ardhi umehakikisha kuwepo na upatikanaji wa miundombinu kwa ajili ya jamii?
  • Je, upimaji huu umeweka kipaumbele kwa watoto kwa kuwapa maeneo ya kuchezea?
  • Je, upimaji huu umelenga kuboresha afya ya jamii kwa kuacha maeneo ya wazi kwa ajili ya kupumzika?
  • Je, upimaji huu umeweka kipaumbele cha kuwa na huduma za kijamii kama vile hospitali na shule, badala ya kusubiri kuendelea kutegemea miji iliyopo karibu?

Lakini ukweli ni kwamba kumekuwa na mapungufu mengi ambayo hayapaswi kufumbiwa macho na serikali inapaswa kuingilia kati ili kuzuia uharibifu wa ardhi na kuendeleza miji inayozingatia vigezo na mipango bora. Baadhi ya changamoto ni pamoja na:
  • Barabara zilizowekwa kwa upana mdogo ambao unazuia magari makubwa kupishana kwa urahisi.
  • Uuzaji holela ambao umesababisha watu kununua viwanja visivyo rasmi au kushuhudia migogoro ya mipaka.
  • Upungufu wa maeneo ya wazi kwa ajili ya jamii kutokana na kuzingatia zaidi faida binafsi badala ya maendeleo ya pamoja ya jamii.
  • Ucheleweshaji wa huduma muhimu kama maji kutokana na kukosekana kwa mipango mizuri ya miundombinu.
  • Kukosekana kwa huduma za msingi kama vile ukusanyaji wa taka na maji taka kutokana na miundombinu mibovu ya barabara.

Mambo ya Kufanyika

Kwa kuzingatia changamoto hizi, hatua zifuatazo zinapaswa kuchukuliwa:

1. Kuweka Alama na Utambulisho wa Maeneo ya Serikali
Maeneo ya serikali yanapaswa kuwekewa alama na kutambulika rasmi ili kuzuia uuzaji holela. Maeneo haya yanapaswa pia kuorodheshwa kwenye tovuti ya ardhi ili kuwa na uwazi zaidi.

2. Kuainisha Matumizi ya Ardhi:
Serikali inapaswa kuainisha maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo, viwanda, na makazi ili kuwa na mipango endelevu na sahihi zaidi. Maeneo haya yanaweza kuorodheshwa kwenye soko la ardhi ambapo litawafikia watu wengi wenye uitaji wa ardhi.

3. Kuandaa Sheria za Kudhibiti Uuzaji wa Ardhi:
Wizara ya Ardhi inapaswa kuandaa sheria madhubuti za kudhibiti uuzaji holela wa ardhi. Soko la ardhi la kidigitali linaweza kuwa suluhisho ambapo mauzo yote yataorodheshwa na kusimamiwa kwa uwazi.

4. Kusimamia Upimaji wa Ardhi:
Serikali inapaswa kusimamia kwa karibu upimaji wa ardhi kuhakikisha maeneo yamepimwa kwa usahihi na kuzingatia mahitaji ya miundombinu kama barabara, maeneo ya wazi kwa watoto, masoko, hospitali, na shule.

5. Kuboresha Utaratibu wa Utoaji wa Hati Miliki:
Utoaji wa hati miliki za ardhi unapaswa kuwa wa haraka na wa uhakika. Matumizi ya teknolojia ya kidigitali yanaweza kusaidia kufanikisha hili kwa kuwa na mifumo inayotambulika kisheria.

6.Soko La Ardhi La Kidigitali
Hili litakuwa soko rasmi ambalo wizara ya ardhi inaweza kuliunda kidigitali kwa lengo la kuraisisha uuzaji na ununuaji wa ardhi ulio mzuri. Mambo ambayo yatafanyika kwenye soko la kidigitali.

•Usajili na Utambulisho: Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa ardhi yote inapimwa na kusajiliwa kwa kupewa namba rasmi za utambulisho. Hii itasaidia kuweka rekodi sahihi za umiliki na kuzuia udanganyifu.

•Akaunti za Kidigitali: Kila muuzaji na mnunuzi wa ardhi wanapaswa kuunda akaunti rasmi kwenye soko la ardhi la kidigitali. Utambulisho rasmi kama vile namba za NIDA au namba ya leseni ya udereva zinapaswa kutumiwa kwa madhumuni ya usalama na uwazi.

•Tangazo la Ardhi: Muuzaji anapaswa kuweka tangazo kwenye soko la ardhi la kidigitali lenye maelezo kamili kuhusu ardhi inayouzwa, ikiwa ni pamoja na namba za utambulisho, thamani ya ardhi, picha za ardhi, na mawasiliano ya muuzaji.

•Mchakato wa Ununuzi: Mnunuaji anaweza kutembelea soko la ardhi la kidigitali ili kutafuta ardhi inayomfaa. Baada ya kuchagua, mnunuaji anapaswa kufuata taratibu zilizoidhinishwa kisheria za mauziano ya ardhi.

•Utengenezaji wa Hati: Baada ya kukamilisha mauziano, taratibu za utengenezaji wa hati ya umiliki wa ardhi zinapaswa kufuatwa. Tangazo la uuzaji linapaswa kutolewa kwenye soko la ardhi ili kuthibitisha mabadilishano.

•Kwa Wamiliki Halali: Wamiliki halali wa ardhi wanaweza kuuza ardhi yao kwenye soko la ardhi la kidigitali kwa kufuata taratibu zilizowekwa. Kwa ardhi ambayo tayari ina hati, taratibu zinazohitajika zinaweza kujumuisha ubadilishaji wa majina ya hati badala ya utengenezaji wa hati mpya.

•Ardhi Vijijini: Kwa ardhi vijijini, muuzaji na mnunuaji wanapaswa pia kufuata taratibu zote za kisheria kama ilivyoidhinishwa na katiba, hata kama mchakato unaweza kuwa tofauti kidogo na maeneo ya mijini.kulingana na ukuaji wa tecnolijia lakini pia serikali iongeze namna bora za kufikisha utoaji wa hati miliki mpaka vijijini.

•Kuhakikisha kuwa mchakato wote unafuata sheria za ardhi na kuzingatia uwazi na usalama ni muhimu sana. Soko la ardhi la kidigitali linaweza kuwa suluhisho bora kwa kuongeza ufanisi na kupunguza udanganyifu katika manunuzi ya ardhi.

FAIDA
  • Kupunguza miji isiyo na mipango na kuongeza usalama wa mazingira ya kuishi.
  • Kupunguza upotevu wa rasilimali za jamii kama maji na kuboresha miundombinu.
  • Kuongeza usalama katika mazingira ya watoto kwa kuwa na maeneo salama ya kuchezea.
  • Kusaidia katika utoaji wa hati miliki za ardhi kwa njia ya kidigitali na kuongeza pato la taifa kupitia kodi.
  • Kupunguza gharama zisizo za lazima kama fidia wakati wa kupisha miundombinu.

Ardhi ni rasilimali muhimu ambayo tunapaswa kuithamini na kuitunza kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom