aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 798
- 1,178
👉 Ardhi ni nini?
👉 Nani anasitahili kuilinda ardhi ya visiwa vya Zanzibar?
👉 Mmiliki ni nani?
👉 Nani anaweza kumiliki?
Kila nchi Duniani ina ardhi yake huenda matumizi ya ardhi katika kila nchi yanaweza kutofautiana kulingana na maamuzi yao.
Nchi zote Duniani zinaamini katika ardhi zao na sio rahisi kugusa ardhi yao kwa namna unavyotaka wewe! Uwe mzawa au mgeni.
Kwa wageni ndio hatari zaidi kuamua tu au kuchukua uwamuzi wao katika kujimilikisha hali ya kuwa ardhi ipo sehemu ambayo ina Kiongozi wake mkuu ambaye ni mkuu wa nchi pamoja na watendaji wengine wa serikali.
Lakini zaidi nchi Ina wananchi ambao ni wazawa na bila shaka wengi wao wanamiliki ardhi kwa namna tofauti.
UKubwa wa Visiwa vya Zanzibar ni 2,461 km².
Je Zanzibar ina mfumo wa ardhi yake ambao unaonyesha matumizi ya ardhi yake ni % ngapi?
Kwa lugha nyingine tafakuri inaweza kusimama katika asilimia ya ngapi ya ardhi ambayo imetumika katika maendeleo ya nchi?
Inawezekana Zanzibar kuna miradi mingi ambayo inatekelezwa na wageni,lakini je hoja ni majengo ambayo wageni wamejenga?
Labda ni sawa kuhoji maeneo ambayo wageni wanayamiliki huku hakuna mradi wowote unaoendelea? yawezekana wageni hao wamekwama kutokana na ile sheria ya serikali ambayo inasema mgeni akinunua ardhi iwe ni kwa ajili ya kuwekeza na sio kuishi tu?
Samahani! 🤚 naomba niwe wazi kidogo katika hiyo sheria, mimi ninaunga Mkono serikali ya nchi ya Zanzibar kwa 100%✊.
Ardhi ya Zanzibar ni ndogo kwa ukubwa wake kama inavyoonekana Ki Jiografia, kwa namna gani ardhi itolewe bila utaratibu maalum? tena kwa vigezo? .
Huenda bado kuna mwanya sehemu ambao unaruhusu wawekezaji FEKI kuamini kwamba wanaweza kumiliki ardhi Zanzibar.
Nani anayewabeba wageni FEKI ambao wanavaa Koti la uwekezaji hapa visiwani Zanzibar?
Yawezekana kuna wageni ambao wanamiliki maeneo na huwakuti ZIPA wala Kamisheni ya Utalii 😳 wageni wa namna hii wanachukuliwa hatua za namna gani?
Kuna shida mahali? au wazawa baadhi wanahusika ?
Nani atainusuru ardhi ya Zanzibar jamani? 😭😭
Shukran 🤝
NOTE: Natarajia kufanya mwendelezo zaidi kuhusu ardhi ya Zanzibar naamini nitapata ushirikiano zaidi kutoka kwenu!