ardhi ye ekari 50 ama zaidi

Chimbuvu

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2012
Posts
4,401
Reaction score
2,341
habari wakuu.ninapenda kujua ama ushauri kuhusiana na kupangilia viwanja.
nina eneo lenye ekari zaidi ya 100 na ninataka kulikata vipande vipande/plots kama 300 hadi 400.
napenda kujua sheria ya ardhi inaniruhusu ikiwa eneo langu lina hati miliki?na kama hairuhusu ni nani anayetakiwa
nimwite aje alikate/kuligawa?
 
Yaani we unamiliki VOGUE halafu hujui utaratibu mkuu? Joke!!!!

Serikali ya Kijiji au Mtaa huwa wanajifanya hizi dili wanashughulika nazo,na wengi nyumba zetu tumejenga kwenye maeneo hayo.Ila eneo lako ni kubwa sana na lazima uwe Salama.

Kwanza Tafuta Local Private Surveyor,hawa watakuwa ni msaada wa mwanzo kwako.Na Serikali za Vijiji na mitaa wanakuwa wanawajua hawa watu,maana huwa wapo nao kwenye miradi kadhaa ya namna hiyo.

Then hawa watakuongoza njia za kupita.
Hao Surveyors wengi wanawajua waliopo wizarani maana ndio wapo nao kwenye utendaji kila siku.
Kisha itaangaliwa taratibu ya kubadilisha matumizi kutoka kwenye shamba kwenda kwenye viwanja vya makazi.

Hakikisha unawashirikisha Serikali ya Kijiji au Mtaa,maana ni msaada mkubwa sana kwako.Maana hata wizarani watatakiwa kuwasiliana nao hao watu na hata watu wote watakaonunua viwanja hivyo lazima wapite kwao.
Ifahamike kwamba Serikali za Mitaa na vijiji zipo kisheria na pia zinaruhusiwa kupeleka mapendekezo ya mabadiliko ya utumiaji wa ardhi pale inapobidi.
 
Nilishafanya hivyo but ilipofika jiji wakasema mpaka wakae kikao cha madiwani ambapo hukaa mara moja kwa miezi 6.na hapo ukimaliza then iende wizara ya ardhi.huu ni mwaka wa pili sasa.hili ndio naona sababu ya makazi holela kuendelea kwa kasi mijini.sheria ya ardhi iangaliwe upya
 
hongera best kuwa na hekari zote hizo nakushauri onana na mwenyekiti au afisa ardhi atakusaidia kwa jambo hilo au ukitaka nenda ofisi za ardhi zilizokaaribu nawe watakushauri namna ya kufanya juu ya hekari hizo

au nenda halmashaurini usikie wao wanasemaje ukimaliza hapo naomba uniuzie nami japo hekari 10 tu nipande matunda yangu hapo kdogo
 
Huko kote nilishapita ladyfurahia kuna plan iliyokuwa na viwaja kama 200,uwanja wa mpira,stand,open space etc nataka jua sheria,maana ndio inayosababisha delay


 
Last edited by a moderator:
Tenga pesa,uone kila kitu kitakuwa sawa.
Maana imekuwa sasa bila Rushwa hatuendi.
Weka fungu lao uone kama kikao hakikaki.

We tafuta Boss mmoja kule Ardhi uone kama habari haiishi.
 
mkuu kwanza hongera sana kwa kuwa na ardhi kubwa , ni hivi we mtu wako muhimu hapa ni surveyor ambaye ameshafanya kazi kama hii ...ukipita mwenyewe utaumia tena vibaya , huyu surveyor kama jamaa walivyosema hapo juu lazima ana mtu wake wizarani , step ya kwanza ni kujua mipango ya serikali kwa eneo hilo kwa hiyo watakuja huku kuchukua vipimo vyao kupeleka wizarani , baada ya hapo sasa ndio wakate hizo plots alafu urudi tena wizarani kwa approval alafu ndo nafikiri stage ya mwisho project yako inaweza fanyika na wewe ukauza I guess ndio mpango wenyewe , vizuri unapouza washirikishe manispaa , so kama plot ya mil 5 mnaweza sema hata mil 6 etc manispaa ndio itangaze kwa wanaotaka viwanja ....hamna sehemu yenye urasimu bongo kama ardhi lakini komaa hii kitu inawezekana kabisa ila andaa hela ndefu kufanikisha .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…