Are democratic reforms at risk in Tanzania? Inside Story

Kuanzia dakika ya 10, Tundu Lissu anasema licha ya kwamba Magufuli alikuwa katili, lakini hakuwahi kuwatwisha tuhuma za ugaidi kama alivyofanya Samia.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nini chachekesha hapa Mkuu?

Je, si kweli kuwa Magufuli alikuwa katili kama ambavyo Lissu amesema? Alikuwa katili mno.

Je, kiongozi gani wa Upinzani katika kipindi cha miaka 6 iliyopita aliwahi kushukiwa juu ya swala la Ugaidi? Hakuna!.
 
Kinachochekesha ni kwamba, licha ya ukatili wa Magufuli, hakuwahi hata siku moja kuwabebesha tuhuma za ugaidi CHADEMA.

Lakini Samia kafanya hivyo.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi kuliko Magufuli.

Kwa maneno mengine, ni kama Lissu anasema hata Magufuli alikuwa na unafuu.

That is what is funny, sir.
 
Kuanzia dakika ya 10, Tundu Lissu anasema licha ya kwamba Magufuli alikuwa katili, lakini hakuwahi kuwatwisha tuhuma za ugaidi kama alivyofanya Samia.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Lisu anatia huruma analialia Kama mtoto wa kambo

USSR
 
Kinachochekesha ni kwamba, licha ya ukatili wa Magufuli, hakuwahi hata siku moja kuwabebesha tuhuma za ugaidi CHADEMA.

Lakini Samia kafanya hivyo.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi kuliko Magufuli.

Kwa maneno mengine, ni kama Lissu anasema hata Magufuli alikuwa na unafuu.

That is what is funny, sir.
Wao kila mtu ni katili hawajui sheria ndio zinawasimamia ,

USSR
 
Inafikirisha..Al Jazeera is owned by Qatar ..Qatar is monarchical state meaning undemocratic...
Qatar according to the press freedom index has less press freedom than TZ. We are in a clown world
 
Kinachochekesha ni kwamba, licha ya ukatili wa Magufuli, hakuwahi hata siku moja kuwabebesha tuhuma za ugaidi CHADEMA.

Lakini Samia kafanya hivyo.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi kuliko Magufuli.

Kwa maneno mengine, ni kama Lissu anasema hata Magufuli alikuwa na unafuu.

That is what is funny, sir.
Hivi Lissu huwaga ana kumbukumbu na kile anakuwa anakiongea?Nakumbuka amewahi kumkejeli baba wa Taifa kuwa aliongoza kiunjaunja,Pia Mkapa aliamini ni dikteta,serikali ya Kikwete akaifananisha na ya makabulu na akaita fascism regime na Mbaya zaidi akatamka hadharani bila hata kupepesa macho Kwa kumuita hayati Magufuli katili dikteta na kwamba Tanzania imepata Rais wa ovyo kuwahi kutokea na saizi anasema Mama Samia ni katili zaidi ya Marais wote kuwahi kuongoza Tanzania.Lissu atoke hadharani anataka nn isije ikawa The agenda behind the Scene
 
Mama Samia hawezi vita chafu za kisiasa, ana hulka ya huruma na sio jeuri, pia ni mtu wa kutazama na kujali perspective ya dunia dhidi yake (Anajali jinsi gani dunia inavyomchukulia), hii tishatisha na kukamata watu ni kuamsha vita ya kisiasa ambayo hatoiweza.

Magufuli hakuwa na hulka ya huruma na alikua jeuri kweli kweli, na alikua hajali dunia inamchukulia vipi na inamsema vipi, ila alikimbizwa mchaka mchaka wa 4G na wanasiasa/viongozi wa dini/haki za binaadamu mpaka ikabidi risasi na watu wasiojulikana watumike.

Unapo pambana au kuanzisha vita chafu za kisiasa, lazima;

1) Uwe na roho mbaya.

2) Uwe Muongo.

3) Uwe tayari kuua na kuteka, bila kujali familia zao watakazo acha nyuma.

4) Uwe muonevu.

5) Uwe huna kujutia.

6) Uwe fisadi (Kununua wanasiasa kwa rushwa, vitisho).

7) Uwe bingwa wa kujitoa ufahamu (Hamnazo).

8) Uwe na kifua cha kuhimili mikiki mikiki na matusi.

9) Usiwe muoga.

10) Usiwe mtu wa kubadilisha maamuzi hata kama umekosea na unajua kwamba umekosea.

Yote haya Mama Samia hana, cha ajabu anaanzisha (Au CCM wanamshauri kuanzisha) varangati chafu za kisiasa asizoziweza. Hao wanao muunga mkono ndani ya CCM muda si mrefu watarudi nyuma na kumwachia mzigo aweweseke nao peke yake.

Subirini moto uwake ndani na nje ya nchi. Mtajionea.

Time will tell, atatulia tu.
 
Kuanzia dakika ya 10, Tundu Lissu anasema licha ya kwamba Magufuli alikuwa katili, lakini hakuwahi kuwatwisha tuhuma za ugaidi kama alivyofanya Samia.

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
😂😂

Anamatatizo?

Kwa hiyo anamsafisha tena mbaya wake..? Siasa bhana!!
 
Demokrasia ya Tanzania imekabidhiwa mikononi mwa wasioijua thamani yake inaelekea kutupwa jalalani.
 
Kinachochekesha ni kwamba, licha ya ukatili wa Magufuli, hakuwahi hata siku moja kuwabebesha tuhuma za ugaidi CHADEMA.

Lakini Samia kafanya hivyo.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi kuliko Magufuli.

Kwa maneno mengine, ni kama Lissu anasema hata Magufuli alikuwa na unafuu.

That is what is funny, sir.
Sidhani kwamba kitendo cha serikali ya Samia kumfungulia Mbowe mashitaka ya ugaidi na tuhuma nzito za kupanga mauaji ya viongozi, inamaanisha kwamba Samia ni katili zaidi kuliko Magufuli.

Inajulikana kwamba Magufuli binafsi alikuwa mara nyingi akitamani hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wapinzani na wengine waliokatisha mbele yake. Kuna wakati alisikika akisema alitamani awe IGP ili awanyooshe watu fulani. Katika kesi ya mauaji ya Akwilina, ilisikika kwamba aliagiza kina Mbowe wafunguliwe kesi ya mauaji ya Akwilina. Kilichozuia hayo hakifahamiki. Mara nyingine alisikika akiagiza kwamba mtu yeyote anayelalamika vyuma vimebana, afunguliwe mashitaka ya kutoa takwimu zake binafsi, maana takwimu za serikali zinasema uchumi inapaa. Hilo nalo halikutekelezwa.
Kinachoonekana hapa rais Samia ana mfumo wa utawala tofauti kidogo na wa Magufuli. Nadiriki kusema Samia, dove, kazungukwa na more powerful Hawks, wakati Hawk Magufuli alizungukwa na very influential doves.

Samia kaahidi mengi ambayo kashindwa kuyatimiza, the Hawks carried the day. Rejea ahadi ya kukutana na wapinzani. Hata hii bajeti yake inaonesha jinsi anavyoyumba na kuyumbishwa na Hawks.
Pamoja na yote hayo, persecution inafanikiwa pale the persecuted wanaogopa. Lakini Mbowe ambaye during Magufuli tyranny alikuwa mostly Dove, sasa anabadilika na kuelekea kwa Lissu. Hata tone yake imebadilika sana. Hawa ndio mashujaa wa kweli wa Tanzania
 
Kongamano la katiba Mwanza liko pale pale
 
Lisu anatia huruma analialia Kama mtoto wa kambo

USSR
Acha kupotosha. Lissu ametumia vizuri sana fursa hiyo kuieleza dunia kinachoendelea. Baada ya risasi 16 kuingia mwilini mwake, na akabaki na chenji ya risasi moja kama trophy, na bado anaunguruma katika platform mbalimbali za kimataifa, na kile kimbunga chake wakati wa kampeni za urais 2020, zilizomtia hofu Magufuli hata akasahau ahadi yake kwa jumuiya ya mataifa kwamba uchaguzi wa 2020 utakuwa wa haki - kuna hata chembe ya kulialia mtu wa aina hiyo? Wewe na ccm yenu ndio mnalialia. Mmejificha nyuma ya magari ya kuwasha na risasi za polisi. Shame to ccm, such a weakling, can't standvon its feet without police support
 
😂😂

Anamatatizo?

Kwa hiyo anamsafisha tena mbaya wake..? Siasa bhana!!
Lissu hajamsafisha mtu. Alichosema tu ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi. Nukuu za ukatili na unyanyasaji wa Magufuli zimetajwa na kila mshiriki wa mjadala huo
 
Sidhani kwamba kitendo cha serikali ya Samia kumfungulia Mbowe mashitaka ya ugaidi na tuhuma nzito za kupanga mauaji ya viongozi, inamaanisha kwamba Samia ni katili zaidi kuliko Magufuli.

Inajulikana kwamba Magufuli binafsi alikuwa mara nyingi akitamani hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya wapinzani na wengine waliokatisha mbele yake. Kuna wakati alisikika akisema alitamani awe IGP ili awanyooshe watu fulani. Katika kesi ya mauaji ya Akwilina, ilisikika kwamba aliagiza kina Mbowe wafunguliwe kesi ya mauaji ya Akwilina. Kilichozuia hayo hakifahamiki. Mara nyingine alisikika akiagiza kwamba mtu yeyote anayelalamika vyuma vimebana, afunguliwe mashitaka ya kutoa takwimu zake binafsi, maana takwimu za serikali zinasema uchumi inapaa. Hilo nalo halikutekelezwa.
Kinachoonekana hapa rais Samia ana mfumo wa utawala tofauti kidogo na wa Magufuli. Nadiriki kusema Samia, dove, kazungukwa na more powerful Hawks, wakati Hawk Magufuli alizungukwa na very influential doves.

Samia kaahidi mengi ambayo kashindwa kuyatimiza, the Hawks carried the day. Rejea ahadi ya kukutana na wapinzani. Hata hii bajeti yake inaonesha jinsi anavyoyumba na kuyumbishwa na Hawks.
Pamoja na yote hayo, persecution inafanikiwa pale the persecuted wanaogopa. Lakini Mbowe ambaye during Magufuli tyranny alikuwa mostly Dove, sasa anabadilika na kuelekea kwa Lissu. Hata tone yake imebadilika sana. Hawa ndio mashujaa wa kweli wa Tanzania
Sawa Kamanda.
 
Mama Samia hawezi vita chafu za kisiasa, ana hulka ya huruma na sio jeuri, hii tishatisha na kukamata watu ni kuamsha vita ya kisiasa ambayo hatoiweza.

Magufuli hakuwa na hulka ya huruma na alikua jeuri kweli kweli, ila alikimbizwa mchaka mchaka na wanasiasa mpaka ikabidi risasi na watu wasiojulikana watumike.

Unapo pambana au kuanzisha vita chafu za kisiasa, lazima;

1) Uwe na roho mbaya.

2) Uwe Muongo.

3) Uwe tayari kuua na kuteka, bila kujali familia zao watakazo acha nyuma.

4) Uwe muonevu.

5) Uwe huna kujutia.

6) Uwe fisadi (Kununua wanasiasa kwa rushwa, vitisho).

7) Uwe bingwa wa kujitoa ufahamu (Hamnazo).

8) Uwe na kifua cha kuhimili mikiki mikiki na matusi.

9) Usiwe muoga.

10) Usiwe mtu wa kubadilisha maamuzi hata kama umekosea na unajua kwamba umekosea.

Yote haya Mama Samia hana, cha ajabu anaanzisha varangati chafu za kisiasa asizoziweza.

Time will tell, atatulia tu.
Well said. Kinachomfanya Samia aonekane katili zaidi ni kule kuyumba kwake. Magufuli alitangaza mapeeeema kabisa kwamba wapinzani ni maadui wake namba 1 na kwamba ana mradi wa kuviteketeza vyama vya upinzani kufikia 2020. Daima aliwatarget viongozi wa upinzani. Hakuna mikutano, hakuna bunge live. Kesi kila kona. Wengi kawanunua. Waliokataa kawatesa sana tu. Kawafilisi fedha zao na mali zao.

Samia je? Kaanza kwa ahadi ya kukutana nao. Kafungulia akaunti zilizofungwa, baadhi kawafutia mashitaka. Lakini hana misingi imara. Kavutwa gauni na watemi ndani ya ccm. Sasa anatenda kinyume kabisa na mwelekeo wa kwanza. Hana msimamo. Ni rais dhaifu sana
 
Kinachochekesha ni kwamba, licha ya ukatili wa Magufuli, hakuwahi hata siku moja kuwabebesha tuhuma za ugaidi CHADEMA.

Lakini Samia kafanya hivyo.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba Samia kaenda mbali zaidi kuliko Magufuli.

Kwa maneno mengine, ni kama Lissu anasema hata Magufuli alikuwa na unafuu.

That is what is funny, sir.
Da hicho kinaweza kuwa kichekesho kweli?
 
Back
Top Bottom