Nasikitika sana kuona kwamba wanaume wa humu ndani wanafurahia kitendo cha wao kutoka nje eti kwa sababu tu wako entitled. Imeandikwa wapi? katika kitabu kipi cha DINI Qoran au Biblia ipi? Hivi huyo aliyeleta hii thread ni mwanamke au mwanamme?
Naomba nikujibu kama ifuatavyo: Are you married? If yes unapohalalisha maneno yaliyoandikwa na mwanadamu aliyezungukwa na upofu, ulemavu wa kufikiri, asiyekuwa na chembe hai ya fikira what is your expectations? If not; imagina una mume anatoka nje ya ndoa na wewe unafurahi kwa sababu ulisoma kitabu kikisema hivyo, where are you? zinduka best ukili mbaya wa maneno uliyowahi kutamka na kuyakubali basi ujue yatakufata mpaka mwisho wa maisha yako.
Wanaume nyie ni vichwa vya familia Imeandika kwenye biblia tangu enzi hizo, hakuna wa kuibadili), kama head of the family unapoenda mrama basi ujue na wafuasi wako wote wametenda dhambi. Wnawake ndiyo nguzo za familia kwenye malezi ya watoto na familia kwa ujumla kama utapotoka eti kwa sababu mumeo anaenda nje na wewe utoke nafikiri utakuwa hujamtendea haki.
Wanawake wengi wamekaa miujiza itendeke bila maombi, siku hizi naona hata kitchen party zinafundisha eti lazima unapoolewa uwe na "KDIMUMU" ili nyumba yao iwe stable, hivi kweli kuna kitabu chochote cha mwenyezi Mungu kinahalalisha UZINZI? Enyi kizazi chenye upofu, fungueni macho muone, acheni kusoma vitabu vinavyopotosha jamii, soma vitabu vyenye mafundisho mema kwa jamii na malezi mema kwa jamii zenu.
Wanaume mnapenda kwenda nje ya ndoa zenu nendetu tu kwa sababu nafsi yako hai haina utii mbele ya mwenyezi Mungu, na kwa kufanya hivyo unajipalia makaa ya moto siku yako ya mwisho. NI vizuri uanze kujifunza kuridhika na ulivyonavyo, kama hana hadhi ya vile unavyopenda ebu mpeleke shule kidogo ya kufanya yale unayopenda ili ujipunguzie hizo dhambi unazojitwika bila sababu. Sdihani kama wanawake tuko dull kiasi cha kutokufundishika. Kaeni chini msome maneno ya Mwenyezi Mungu mjue ni wapi mmepotoka, maisha yende vizuri.
Mwanajamii1 sijapenda thread yako, haina mafundisho yoyote kwa jamii zaidi ya kupotosha na kuchochoea vijitabia vya kizinzi kwa wanaume. Ona wote walivyokuitikia as if ndiyo umekubaliana nao kwa wao kufanya hivyo. Kabla ya kutoa thread angalia sana inawezaje kuokoa kizazi hiki chenye laana ya tamaa za mwili, fikra ndogo, kutokuwa n autii kwa nafsi zao wenyewe na Mungu?
Kama unaweza kusoma hizo novel zako zenye mafundisho ya hivyo basi soma hiki nacho ili uje ubatilishe lile unalosema hapa. THE WOMAN OF PROVERB 31" tuletee feedback hapa ili wajue who is a woman and its responsibilities to the family. Kama wewe ni wa kike basi utajua kosa lako liko wapi kuleta thread kama hii.
Nisamehe kama nimekukwaza! that is the reality!