Argentina atinga Kombe la Dunia kibabe; awahi Marekani/Canada na Mexico kulitetea

Argentina atinga Kombe la Dunia kibabe; awahi Marekani/Canada na Mexico kulitetea

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,350
Reaction score
26,166
Mabingwa wa soka wa dunia, timu ya taifa ya Argentina, leo alfajiri imefuzu mashindano ya kombe la dunia ya mwakani kwa kuibamiza Brazil mabao 4-1. Mashindano hayo ya mwakani yatapigwa kwenye nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico.

Baada ya ushindi wake huo, Argentina amefikisha alama 31 ambazo haziwezi kufikiwa na timu iliyopo nafasi ya saba (Venezuela) au ya nane (Bolivia) zenye alama 15 na 14 mtawalia. Mpambano wa kufuzu huko Amerika ya Kusini unajumuisha mataifa 10.

Baada ya mechi 18 (kwasasa zimebaki 4 tu), mataifa sita ya juu hufuzu moja kwa moja kombe la dunia huku nafasi ya saba akigombea nafasi moja na mshindi wa Ocenia. Hadi sasa, Argentina anaongoza ukanda huo wa Amerika ya Kusini kwa alama 31 ambazo zimempa nafasi ya kufuzu moja kwa moja.

Wakiwa bila Messi jana na mechi iliyotangulia, waliwapoteza kabisa Brazil na kufanikiwa kuwaadhibu vikali kupitia kwa McAlister, Enzo, Alvarez na Simeone. Bao la Brazil lilifungwa na Cunha. Ni rasmi sasa bingwa mtetezi Argentina amewahi kwenda kulitetea kombe lake alilolitwaa nchini Qatar mwaka 2022 kwa ushindi dhidi ya Ufaransa.
 
Wale jamaa ni kama kosi la Wahuni wa barabarani au panya road. Timu Yao wengi hawacheki na kima, siyo wapaka poda kabisa na hawana ubishoo Wala utoto wa mama, ni wasela na Wahuni watupu.
 
Back
Top Bottom