Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Hii leo ndio mechi, kesho inajulikana nani atapigwa za kutosha.
Croatia wapo vizuri, Argentina wapo vizuri, Dk 90 zitaamua, Lakini naiona Argentina na France fainali.
Kabla hauja bet tayari ushaliwa pesa zako.
Leo andunje anarudi kwao, kesho wamatumbi wa Paris nawao wanarudi kwao.

Fainal Morocco vs Croatia.

Morocco 1 Croatia 0
 
Magoli manne mnayoyapigia kelele ndo hayo ya penati?

Na Argentina ilipaswa iwe na magoli 10 endapo asingekosa ile penati siku ile

Rekodi nyingine ambayo hujaiweka ni kuwa Messi ndio mchezaji pekee aliyepewa penati nyingi

Kingine Messi ana on target 13 sio 22 kama ambavyo unataka kutuongopea hapa

Umeandika uongo mtupu, eti Messi ndio anayeongoza kwa kutengeneza nafasi kuliko mchezaji yeyote

Nani kakudanganya?

Griezman unamuweka nafasi ipi?

XG Mbappe ana 3.37 na XA ana 1.23 bado sioni sababu ya kum praise sana Messi kumuweka katika daraja la peke yake.

Na bado anaongoza kwa goli 5 ambazo hizo kazipata kupitia jitihada zake binafsi na sio penati

Messi kazidiwa factors nyingi na wachezaji tofauti tofauti ila ndio hivyo hawasikiki kwasababu hawajatengeneza fame ya kufanya wazungumziwe.
 
Scarrs hampendi tu Messi, hana sababu
 
Huyo ana chuki zake binafsi tu zinamsumbua saivi anatapatapa tu haoni pa kujificha
Huwa nakereka sana kuona mtu anamuita mwingine hater kwasababu ya criticism

Nyinyi mkimkosoa Ronaldo mnakuwa mnajua mpira, sisi tukimkosoa Messi tunakuwa haters???

Sasa angalau ungefanya hata udadisi wa hicho alichokiandika kama kina ukweli wowote kabla ya kufikia kuniita hater

Hujataka kujisumbua kudadisi kwasababu tayari upo katika upande wake anao support

Mashabiki wa Messi sijui mna tatizo gani?

Walau mwenzako amejitokeza kunipinga kwa data (ambapo zipo na data fake kati ya hizo)

We unakuja moja kwa moja kuniita hater, sijapenda kiukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…