Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Naona kama kipa aliruka na kadondoka mwenyewe vibaya ilitakiwa iwe goli
 
Nilishangaa sana inakuwaje Kounde anacheza huku amevaa cheni..!Ubishoo uliopitiliza
Niliona clip ya goal la marehemu Boupa Diop, alipovua shati alikuwa amevaa cheni. Nikajiuliza kumbe zamani walikuwa wanaruhusiwa kuvaa hiyo mikufu, huenda siku hizi wameanza kuikataza kama huyo Kounde kavuliwa
 
Mimi sio mfuasi wa spain ila mpira wao wanaweza kushinda mechi yeyote

Wanakosa maturity ya timu tu

Kushinda kwa morocco inawezekana ila itakuwa km suprise
Kwa Form waliyokuwa nayo Morocco kwenye michuano hii haitokiwa surprise kushinda.Ukitaja timu tatu zilizo perform vizuri WC hii Morocco ipo.
 
Hawa ufaransa wanavyocheza kule mbele mbona kama vile siwaelewi, unaweza kuhisi Wana maelekezo kabisa ya kumpa mpira Mbape pindi wanapoenda kushambulia

Movement nyingi Giroud ndio anakuwa kwenye position nzuri ila hapewi mpira anatafutwa Mbape alipo au ndo kusema wachezaji wenzie hawamuamini au vipi

Na hasa kama mpira umetokea Kwa Hernandez ndio kabisa, ye mipira yote anapiga v pass ili kumtafuta Mbape na hapigi pass kwenda Kwa Giroud

Nimeona pia mara kadhaa kutokea upande wa Griezman pia, isije kuwa ufaransa nawao wanataka kutengeneza Ronaldo au Messi wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…