Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Argentina yatwaa ubingwa Kombe la Dunia - Qatar 2022

Iran na USA ndio kitawaka USA atoboi tuko apa natabiri iyo mechi kadi nyekundu lazma zitembe
1998
Screenshot_20221119-130022.png
 
1668856842256.png


1668856585574.png


Kombe la dunia ndio hilo linaanza kugombewa Kesho kwenye ufunguzi wa mashindano hayo yatakayofanyika Qatar.
Mechi ya kesho ni ya ufunguzi ambapo wenyeji Qatar watakuwa wakimenyana na timu ya taifa la Ecuador

Uwakilishi
  • Africa (CAF): 5
  • Asia (AFC): 5 pamoja na mwenyeji inakuwa 6
  • Europe (UEFA): 13
  • North/Central America & Caribbean (CONCACAF): 4
  • Oceania (OFC): 2
  • South America (CONMEBOL): 5
Africa (CAF)
Mataifa ya Afrika itawakilishwa na timu 5 ambazo ni (kwenye mabano ikionyesha nafasi kwenye ranking ya FIFA)
  1. Cameroon (43)
  2. Ghana (61)
  3. Morocco (22)
  4. Senegal (18)
  5. Tunisia (30)
Asia (AFC)
Bara hili linawakilishwa na timu 6 ambazo ni (kwenye mabano ikionyesha nafasi kwenye ranking ya FIFA)
  1. Australia (38)
  2. Iran (20)
  3. Japan (24)
  4. Qatar (50) (hosts)
  5. Saudi Arabia (51)
  6. South Korea (28)
Ulaya (UEFA)
Mataifa ya Ulaya yanawakilishwa na timu 13 ambazo ni (kwenye mabano ikionyesha nafasi kwenye ranking ya FIFA)
  1. Belgium (2)– Mshindi wa 3, 2018 (World Cup best)
  2. Croatia (12) – Mshindi wa 2, 2018
  3. Denmark (10) – Robo fainali 1998
  4. England (5)– Bingwa, 1966
  5. France (4) – Bingwa 1998, 2018
  6. Germany (11)– Bingwa 1954, 1974, 1990, 2014
  7. Netherlands (8) – Mshindi wa 2, 1974, 1978, 2010
  8. Poland (26)– Mshindi wa 3, 1974, 1982
  9. Portugal (9)– Mshindi wa 3, 1966
  10. Serbia (21)– Mshindi wa 4, 1930*, 1962*
  11. Spain (7)– Bingwa 2010
  12. Switzerland (15)– Robo fainali 1934, 1938, 1954
  13. Wales (19)– Robo fainali 1958
Taifa la Italia ni mojawapo ya timu iliyoshanganza wengi kushindwa kwenye micuano ya mchujo pamoja na kuweza kubeba kombe la ligi ya timu za Ulaya msimu uliopita.

Amerika ya kati, kaskazini na Visiwa vya Caribean (CONCACAF)
Wawakilishi ni wanne ambao ni (kwenye mabano ikionyesha nafasi kwenye ranking ya FIFA)
  1. Canada (41)
  2. Costa Rica (31)
  3. Mexico (13)
  4. United States (16)
Oceania (OFC)
  • None qualified
South America (CONMEBOL)
Wawakilishi ni wanne ambao ni (kwenye mabano ikionyesha nafasi kwenye ranking ya FIFA)
  1. Argentina (3)
  2. Brazil (1)
  3. Ecuador (44)
  4. Uruguay (14)
Makundi yamepangwa kama ifuatavyo

Group A:
  1. Qatar,
  2. Ecuador,
  3. Senegal,
  4. Netherlands
Group B:
  1. England,
  2. Iran,
  3. USA,
  4. Wales
Group C:
  1. Argentina,
  2. Saudi Arabia,
  3. Mexico,
  4. Poland
Group D:
  1. France,
  2. Australia,
  3. Denmark,
  4. Tunisia
Group E:
  1. Spain,
  2. Costa Rica,
  3. Germany,
  4. Japan
Group F:
  1. Belgium,
  2. Canada,
  3. Morocco,
  4. Croatia
Group G:
  1. Brazil,
  2. Serbia,
  3. Switzerland,
  4. Cameroon
Group H:
  1. Portugal,
  2. Ghana,
  3. Uruguay,
  4. South Korea
Muda wa michuano
Michuano ya fainali za Kombe la dunia kule Qatar itaanza tarehe 20/11/2022 na kumalisika tarehe 18/12/2022
Yatafanyika wapi?
Mashindano yatafanyika katikla nchi ya Qatar katika viwanja 8 kama ifuatavyo:
  1. Al Bayt Stadium,
  2. Khalifa International Stadium,
  3. Al Thumama Stadium,
  4. Ahmad Bin Ali Stadium,
  5. Lusail Stadium,
  6. Stadium 974,
  7. Education City Stadium
  8. Al Janoub Stadium.
Wimbo maalum wa Kombe la Dunia 2022 - Qatar






Uwakilishi kwa Ligi
  • Ligi ya Uingereza al amarufu kama EPL imewakilishwa na jumla ya wachezaji 134 huku kila timu ikitoa angalau mchezaji mmoja. Timu ya Man City ndio timu yenye wachezaji wengi ikiwakilishwa na wachezaji 16 huku mhasimu wake wa karibu Man United akifuata na wachezaji 14
  • Ikifuatiwa na Laliga iliyowakilishwa na wachezaji 84. Barca 16 na Real Madrid 13, huku timu za Girona and Elche zikiwa hazina mwakilishi hata mmoja
  • Bundesliga inafuatia ikiwa na wachezaji 73 huku Bayern Munich ikiwakilishwa na wachezaji 17
  • Serie A (66)
  • Ligue 1 (52),
  • MLS (35)
Mchezaji mzee ni Alfredo Talavera akichezea Mexico kama golkipa wa akiba ambaye ana miaka 40
Mchezaji kinda ni Youssoufa Moukoko ambaye ni raia wa Kameruni lakini ataicheza timu ya Ujerumani. atafikisha miaka 18 tarehe 20 Nov siku ambayo mashindano haya yanaanza
Mchezaji wa Chelsea Thiago Silva ndiye mchezaji mzee akiwa na miaka 38 kutokea EPL
Mchezaji kinda wa Man United Facundo Pellistri (miaka 20) ndie mchezaji mwenye umri mdogo kutokea EPL

Tangu yaanzishwe mwaka 1930 haya mashindano yameshafanyika mara 23 kama ifuatavyo
(Hii ni pamoja na mashindano yajayo 2022 Qatar na 2026 Marekani)
AFC mara 2
South Korea- Japan 2002, Qatar 2022
CAF mara 1
South Africa 2010
CONCACAF mara 4
Mexico 1970, Mexico 1986, United States 1994, Canada -Mexico -United States 2026
CONMEBOL mara 5
Uruguay 1930, Brazil 1950, Chile 1962, Argentina 1978, Brazil 2014
OFC mara 0
UEFA mara 11
Italy 1934, France 1938, Switzerland 1954, Sweden 1958, England 1966, Germany 1974, Spain 1982, Italy 1990, France 1998, Germany 2006, Russia 2018

Bingwa wa kwanza wa haya mashindani ni Uruguay mwaka 1930
Bingwa wa hivi karibuni ni Ufaransa mwaka 2028

Timu za Afrika zilizofanya vizuri
Hakuna timu ya Afrika iliyowahi kufika hata nusu fainali
Cameroon iliwahi kufika Robo Fainali mwaka 1990
Ghana iliwahi kufika Robo Fainali mwaka 2010
Senegal nayo iliwahi kufika Robo Fainali mwaka 2002

Nafasi ya kila timu kutokana na ranking za FIFA
1. Brazil (1) Bingwa mara 5 1958, 1962, 1970, 1994, 2002
2. Belgium (2)– Mshindi wa 3, 2018 (World Cup best)
3. Argentina (3) Bingwa mara 2 1978, 1986
4. France (4) – Bingwa mara 2, 1998, 2018
5. England (5)– Bingwa, 1966
6. Italy (6) sio mshiriki Bingwa mara 4 1934 *, 1938, 1982, 2006
7. Spain (7)– Bingwa 2010
8. Netherlands (8) – Mshindi wa 2, 1974, 1978, 2010
9. Portugal (9)– Mshindi wa 3, 1966
10. Denmark (10) – Robo fainali 1998
11. Germany (11)– Bingwa mara 4 1954, 1974, 1990, 2014
12. Croatia (12) – Mshindi wa 2, 2018
13. Mexico (13)
14. Uruguay (14) Bingwa wa kwanza 1930 na bingwa tena 1950
15. Switzerland (15)– Robo fainali 1934, 1938, 1954
16. United States (16) Nafasi ya tatu 1930
17. Colombia (17) sio mshiriki
18. Senegal (18)
19. Wales (19)– Robo fainali 1958
20. Iran (20)
21. Serbia (21)– Mshindi wa 4, 1930*, 1962*
22. Morocco (22)
23. Peru (23) sio mshiriki
24. Japan (24)
25. Sweden (25) Sio mshiriki
26. Poland (26)– Mshindi wa 3, 1974, 1982
27. South Korea (28)
28. Chile (29) Sio mshiriki
29. Tunisia (30)
30. Costa Rica (31)
31. Nigeria (32) Sio mshiriki
32. Urusi (33) Sio mshiriki
33. Austria (34) Sio mshiriki
34. Czechia (35) Sio mshiriki
35. Hungary (36) Sio mshiriki
36. Algeria (37) Sio mshiriki
37. Australia (38)
38. Misri (39) Sio mshiriki
39. Scotland (40) Sio mshiriki
40. Canada (41)
41. Norway (42 Sio mshiriki
42. Cameroon (43)
43. Ecuador (44)
44. Uturuki (45) Sio mshiriki
45. Mali (46) Sio mshiriki
46. Paraguay (47) Sio mshiriki
47. Ivory Coast (48) Sio mshiriki
48. Jamhuri ya Ireland (49) Sio mshiriki
49. Qatar (50) (hosts)
50. Saudi Arabia (51)
51. Ghana (61)

Ubashiri wa timu zitakazosonga mbele hatua ya makundi (Ubashiri huu ni kwa mujibu wa wachambuzi wengi wa soka)

Group A
  1. Netherlands
  2. Ecuodor
Group B
  1. England
  2. USA
Group C
  1. Argentina
  2. Poland
Group D
  1. France
  2. Denmark
Group E
  1. German
  2. Spain
Group F
  1. Belgium
  2. Croatia
Group G
  1. Brazil
  2. Switzerland
Group H
  1. Portugal
  2. Uruguay
 
Usa amewekeza sana sasa kwenye football tofauti na tisini kurudi nyuma

USA vs Iran haitakuwa mechi ya kiufundi itakuwa direct football

Kisaikolojia iran ataingia akiwa amepanik hii inaweza kupelekea kupata kadi nyekundu
Wakupaniki atakuwa USA mkuu, sababu iran kwanza atakuwa na mashabiki wengi mana waislamu wenzake wale apo Qatar. Akishika mpira shangwe linakuwa la kutosha

USA lazm apagawe mana anajua akifungwa ni aibu, iran itajiamini mana ata wachezaji wake wengi sio wakubwa kama USA mfani mzuri ni

Urusi na Ukraine bila shaka unaona urusi kinacho mpata
 
Back
Top Bottom