Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mwimbaji, Ariana Grande ameingia tena katika mvutano na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu matumizi ya muziki wake.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alidai kwamba nyimbo zake zisitumike tena katika machapisho yao.
Tukio hilo lilianza wakati akaunti rasmi ya Team Trump, inayomilikiwa na timu ya rais wa Marekani, ilipotumia wimbo maarufu wa Ariana Grande, “We Can't Be Friends (Wait for Your Love),” kama muziki ambatanishi (backgroubd music) katika video ya TikTok yenye ujumbe uliochukuliwa kuwa wa chuki dhidi ya watu waliobadili jinsia.
Katika video hiyo, rais wa Marekani anaonekana akitembea kuelekea kwenye jukwaa, huku maneno yakionekana yakisema: “Mimi na ukweli wangu tunakaa kimya…”
“Wanaume hawawezi kuzaa watoto na hawapaswi kamwe kushindana katika michezo ya wanawake.” Maelezo yaliyoambatana na video hiyo yalisema: “Hili halipaswi kuwa suala la utata,”.
Hii si mara ya kwanza kwa Ariana kulaani matumizi ya muziki wake katika machapisho ya utawala wa Trump, kwani tukio kama hilo lilitokea pia mwezi Juni mwaka huu.