Arif Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, ameshauri serikali kuchakata gesi iwe Diesel na Jet Fuel

Arif Premji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, ameshauri serikali kuchakata gesi iwe Diesel na Jet Fuel

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416

Mbunge wa Mtwara Vijijini Mheshimiwa Arif Premji ameshauri serikali kuchakata gesi iwe Diesel na Jet Fuel, Akiwa anachangia Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Nini maoni yako?

"Tunaongelea mradi wa LNG wa Tirilioni mia moja tril 100. Chombo cha habari cha Citizen na Reuters ya London, kilichapisha habari tarehe 27 mwezi wa kwanza mwaka huu, na kwenye habari hiyo ilimnukuu moja ya Waziri akisema kwamba mkataba utasainiwa mwezi wa sita mwaka huu(2026). Na jana tumesikia kwamba bado kuna majadiliano bado, ipi kauli ya Serikali kuhusiana na kusainisha mkataba huo? Asanteni sana. " Aliuliza Mbunge.

Kuhusiana na Swali hilo Serikali imesema mradi wa LNG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba. Kwamba Mradi wa LNG wa shilingi trilid 100 wakaribia kuanza, Hakuna zuio la kisheria wala kikanuni linalofanya mradi huo usitekelezwe.

" Mradi wa NLG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba ili waweze kusaini mkataba na kuanza mradi huu" Amesema Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba.

Naye Dkt. Nchemba akijibu swali swali Bungeni Aprili 9, 2026, alisisitiza kuwa Serikali inaweka umakini wa hali ya juu kutokana na ukubwa wa uwekezaji huo ambao Tanzania haijawahi kuingia nao. Majadiliano sasa yako hatua za mwisho, yakihusisha masharti muhimu kama angalau asilimia 3 ya gesi kubaki nchini kwa matumizi ya ndani na ushiriki wa makampuni ya wazawa.

Alibainisha kuwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yanasisitiza uchumi shirikishi unaowawezesha wazawa kunufaika moja kwa moja.
 
View attachment 3570639
Mbunge wa Mtwara Vijijini Mheshimiwa Arif Premji ameshauri serikali kuchakata gesi iwe Diesel na Jet Fuel, Akiwa anachangia Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Nini maoni yako?

"Tunaongelea mradi wa LNG wa Tirilioni mia moja tril 100. Chombo cha habari cha Citizen na Reuters ya London, kilichapisha habari tarehe 27 mwezi wa kwanza mwaka huu, na kwenye habari hiyo ilimnukuu moja ya Waziri akisema kwamba mkataba utasainiwa mwezi wa sita mwaka huu(2026). Na jana tumesikia kwamba bado kuna majadiliano bado, ipi kauli ya Serikali kuhusiana na kusainisha mkataba huo? Asanteni sana. " Aliuliza Mbunge.

Kuhusiana na Swali hilo Serikali imesema mradi wa LNG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba.

" Mradi wa NLG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba ili waweze kusaini mkataba na kuanza mradi huu"
Huyu nadhani mgeni na mifumo ya utawala ya nchi
 
Vyombo vyetu vya ndani havilizungumzii hilo kwa kina na ifafanuzi ili wananchi tulijue ila vya nnje ndio vinalizungumzia sana. Hao mabeberu hawata tupiga kweli? Sisi hatuna wataalamu wa ndani ya Nchi walifanyie kazi tubakie kuagiza mitambo tu?
 
Back
Top Bottom