View attachment 3570639
Mbunge wa Mtwara Vijijini Mheshimiwa Arif Premji ameshauri serikali kuchakata gesi iwe Diesel na Jet Fuel, Akiwa anachangia Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu.
Nini maoni yako?
"Tunaongelea mradi wa LNG wa Tirilioni mia moja tril 100. Chombo cha habari cha Citizen na Reuters ya London, kilichapisha habari tarehe 27 mwezi wa kwanza mwaka huu, na kwenye habari hiyo ilimnukuu moja ya Waziri akisema kwamba mkataba utasainiwa mwezi wa sita mwaka huu(2026). Na jana tumesikia kwamba bado kuna majadiliano bado, ipi kauli ya Serikali kuhusiana na kusainisha mkataba huo? Asanteni sana. " Aliuliza Mbunge.
Kuhusiana na Swali hilo Serikali imesema mradi wa LNG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba.
" Mradi wa NLG upo katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya kisheria na kimkataba ili waweze kusaini mkataba na kuanza mradi huu"