Arnold Kayanda Yuko BBC Sasa

Arnold Kayanda Yuko BBC Sasa

JAYJAY

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2008
Posts
8,191
Reaction score
8,490
nilikuwa najiuliza huyu jamaa sijamsikia muda yuko wapi. leo nimemsikia muda mfupi uliopita kwenye taarifa ya habari ya BBC. Taarifa ndio hiyo wadau!

Habari njema kwa mashabiki wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha Radio Clouds FM, Arnold Kayanda ni kuwa hivi karibuni ataanza kusikika
tena Radioni baada ya kujiunga na Shirika la Utangazaji la BBC Swahili.

Kayanda ambaye amejipatia umaarufu zaidi kupitia vipindi mbalimbali vya Clouds kikiwemo kipindi cha Top 20 pamoja na Jahazi, ameitoa habari
njema kwa wasikilizaji wake kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Huu ndio ulikuwa ujumbe wa kwanza alioandika jana: "Siku yangu ya kwanza katika #BBCSwahili. Miongoni mwa walionipokea ni dada yangu Regina Mwalekwa. Hapa tukiwa na ndugu yetu
Baruan Muhuza (kushoto). Picha nikiwa na wanafamilia wengine itafuata hivi punde." Aliandika chini ya picha aliyopiga na Baruan Muhuza na Regina Mwalekwa.

Na hiki ndicho alichokiandika leo baada ya kupost picha hii (hapo juu): "Watu hawa (wengine hawapo pichani) walinipokea vizuri hadi
nikaogopa pengine wameshanitafutia mteja wanasubiri nilale waniuze. Hii ni familia yangu mpya. Shukrani sana Dada Liz Massinga, John Solombi,
Dada Halima Nyanza, Leonard Mubali, Dada Regina Mwalekwa, Hassan Mhelela, Dada Regina Joseph, Ben Mwang'onda, Eric David Nampesya, Baruan
Muhuza na wengine wote. Mungu ameshanifikisha nchi ya ahadi kilichobaki ni kumtumikia. Sasa vijana waambie vijana wenzenu nao wawaambie wenzao
katika ratiba zao watenge muda wa kuisikiliza Idhaa ya Kiswahili ya
‪#‎BBC‬."

Kayanda ameungana na Regina Mwalekwa ambaye pia amejiunga na kituo hicho cha kimataifa hivi karibuni akitokea Clouds FM.

Chanzo: Bongo5
 
Hongera zake.
Mbwiga na Bonge wajitahidi huenda na wao wakachukuliwa na BBC.
 
Duh sikuiz kwenda BBC inaonekana imekuwa easy, hadi watu wa kawaida wanaenda
 
Anorld Kayanda anavyo vigezo vya kuenda BBC. sitazungumzia kielimu, ila ule u-presentation wake na sauti akiwa anatangaza ni ambao unaweza kusikilizwa na hata na watu wenye hekima zao. tofauti na watu kama mchomvu na mbwiga.

Hivi huyu mbwiga ni mtangazaji au mchekeshaji tu kawekwa pale apate pesa kula?

Hizi ni salam kwa Kibonde anayetaka akitawale kipindi kufunika nyota za wenzake, lakini ajuwe wakitakiwa maprofesheno kwenda redio kubwa yeye atabaki clouds mpaka kifo chake.
 
Me napenda tu sauti yake doooh. Millard naamini soon na yeye ataitwa tu BBC

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
target ya kila mtangazaji bongo ni kwenda bbc swahili..inaonekana bbc swahili inajitegemea co bbc world tunayoijua
 
Baruan Muhuza TBC walimzengua akajiendea zake star tv kinyoonge. Mungu si athumani mara kaibukia bibisii uingeredha. Usicheze kabisa na riziki ya mtu, mungu akikuandikia hata wafanyeje wee ni wa kutusua tu.
 
Kuitwa BBC ni kigezo cha mafanikio? Mbona Pasco hayuko BBC na anaingiza mpunga wa maana na ile kampuni yake ya PPR? Pasco hana time na maredio yenu ya kitumwa. Tena nawaambia afadhali ya DIDA au Rose Chitala wana amani bongo kuliko hao kina regina na Kaganda huko UK
 
Last edited by a moderator:
Baruan Muhuza TBC walimzengua akajiendea zake star tv kinyoonge. Mungu si athumani mara kaibukia bibisii uingeredha. Usicheze kabisa na riziki ya mtu, mungu akikuandikia hata wafanyeje wee ni wa kutusua tu.

Kibonde atakuwa mkurugenzi wa ile redio ya Le mutuz
 
Back
Top Bottom