GE2025 Arnold Mvamba: Asitokee Mpuuzi yeyote akasema kwamba Tarehe 29 Oktoba hatutatiki

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wanachama na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanajiamini sana, yaani wanatoa kauli chafu hadharani bila hofu ila angekuwa ni mwanachama wa chama fulani au mwananchi mwenye harakati zake hapa angeambiwa wanaleta Taharuki

Kulingana na kauli ya huyu jamaa ni kwama ukidai haki yako ya msingi au ukikemea maovu wewe ni Mpuuzi

--------------
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Arnold Mvamba, ametoa wito kwa vijana w akiwataka wasikubali kuathiriwa na taarifa za kupotosha zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwavunja moyo na kuwazuia kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao

Akizungumza leo Jumapili 21 Septemba 2025 wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Lumuli, Wilaya ya Iringa, Mwenezi Mvamba amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa zenye kuleta , taharuki , hofu na propaganda zinazolenga kuwakatisha tamaa wananchi, hasa vijana, ili wasijitokeze kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025

Alisisitiza kuwa CCM itaendelea kusimamia amani, umoja na maendeleo ya Watanzania wote, huku akiwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, kutafuta maarifa sahihi na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi

Attachments

  • 2025-09-23-185249930.mp4
    3.4 MB
Back
Top Bottom