Niwape mfano wangu mwenyewe nitembelewapo na wakwe nyumbani kwangu:
Akija mama mkwe, mke wangu anachangamka sana na wanatumia muda wao mwingi jikoni, mie nakuwa 'mpole' throughout.
Akija mamangu mzazi, mke wangu anaishi 'kwa tahadhari' throughout, na anakuwa hajiamini kama hajamuudhi mamangu. Atataka maoni yangu kwa mambo aliyoongea au kumfanyia mamangu kama "Pale niliposema hivi mama hajaudhika kweli?" au "Chakula changu mama hajakipenda nini, mbona kala kidogo sana?"
Akija baba mkwe, mimi na baba mkwe tunachangamka kuliko, tunazungumza kwa vicheko hadi usiku mkubwa, mke wangu anakuwa mpole ajabu na anageuka waiter wa kuhakikisha vinywaji havipungui mezani hadi babake aseme 'up'!
Akija babangu mzazi hali ni hiyohiyo kama inavyokuwa kwa baba mkwe
Mpaka hapo kwa case yangu tu, naona tatizo liko kwenye jinsia ya kike na si kwenye uhusiano wa 'ukwe'.