Arsenal kuitangaza Rwanda msimu huu

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
ARSENAL imeongeza mdhamini mwingine katika jezi zao za MSIMU WA 2018/2019

RWANDA TOURISM watakuwa kwenye jezi za arsenal kwa msimu mzima, NAIONA RWANDA IKIFAIDIKA MARADUFU katika Utalii na kuingiza mamilioni,

Rwanda hawana cha kutuzidi Tanzania kwenye Swala la Utalii,

Tanzania bado tunakimbizana na WAPINZANI
 
Hela ya ruzuku anayo kula Mbowe ingeelekezwa huku pengine tungekuwa tunawadhamini Man city
 
Huku bado tunakimbizana na chaguz ndogo na ununuz wa madiwan
 
Sisi tuna vivutio vingi sana ila sera mbovu, viongozi wao wanaangalia kukusanya kodi na gharama za mipakani.

Tungeweka Sera nzuri na kuwekeza vizuri na kuzisaidia taasisi binafsi hakika watalii wangezidi milioni 10 kila mwaka.

Sisi ni wajinga
 
tukimaliza kuwashughulikia wanaoikosoa serikali tutaliangalia hilo........... sema tatizo niliapa sitasafiri kwenda uraya hizo fursa achaneni nazo, sisi tuna gesi, viwanda na bombadie na tuna ukuta wa mererani.
 
Rais wa Rwanda Shabiki wa Arsenal naona ameona aitumie fursa hiyo kuiletea mema nchi yake... kama Qatar, Etihad, Turkish nk wafanyavyo
 
Uzuri ni kwamba hakuna watakachoenda kuona Rwanda zaidi ya wale manyani na makaburi ya watu walio uwawa kwenye mauaji ya kimbari,cha msingi hapo ni kuteleza tu..tuongeza katangazo kadoogo katakako onesha kwamba Rwanda ni Karibu na Tanzania kwenye kilimanjaro,ngorongoro na Serengeti.
 
Huku viongozi wetu hata kwenda nje kuiuza Tz huko hawajawahi.
Utalii utaongezekea wapi kama hamjitangazi dadek tutasubiri sana
Hata tukitoa fedha kujitangaza ni sisi tunaolaumu leo tutaanza kulalamika kwa nini hizo fedha zisipelekwe kwenye afya au kilimo kitafaidisha Watanzania wengi
 
Hata tukitoa fedha kujitangaza ni sisi tunaolaumu leo tutaanza kulalamika kwa nini hizo fedha zisipelekwe kwenye afya au kilimo kitafaidisha Watanzania wengi
Okey sawa
 
Hata tukitoa fedha kujitangaza ni sisi tunaolaumu leo tutaanza kulalamika kwa nini hizo fedha zisipelekwe kwenye afya au kilimo kitafaidisha Watanzania wengi
Wanasiasa wapo kama sigara kali. Kipindi cha nyuma nchi ilikuwa haina ndege, wameponda sana. Haya kaingia jamaa kazinunua, sasa hivi wanakuambia bora ela uipeleke, kuboresha elimu na ndio maana sometimes taifa linapofanya maamuzi yanahusiana na maswala ya kiuchumi, lisiwasikilize wanasiasa watawavuruga na hujui kesho watasema nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…