watoe hao forbes, mapato ya vilabu je?
kama man city, arsenal, spurs etc wanatangazo mapato madogo compare na kina barca, madrid, man u je na hizo club zimehongwa zitoe mapato kidogo?
hivi na akili zako timamu unaamini timu kama spurs ambayo ndo kwanza inajenga uwanja, timu kama arsenal ambayo mpaka leo haijamaliza deni la uwanja inakaba wachezaji iwalipe mishahara midogo na timu kama man city ambayo hata uwanja haina inategemea uwanja wa jiji la manchester na uwanja wenyewe haujai umepewa nickname emptihad zinaweza kweli kuwa na hela kushinda barca madrid na man u?
ukiangalia source za hela za mpira
1. uwanja, barca madrid na man u zina viwanja vikubwa zaidi
2. idadi ya mashabiki timu hizo tatu kubwa zinao wengi zaidi
3. mauzo ya jezi yametawaliwa na messi, ronaldo, zlatan, neymar, pogba, de gea etc
4. deal kubwa za jezi duniani utasikia ni adidas man u na madrid, barcelona nike etc
sasa kama kila source za revenue wametawala hao mabwana wakubwa hebu tumia angalau asilimia moja ya akili yako uniambie totenham, arsenal au city wamefanya nini wawapite hao.
Eti arsenal inalipa mishahara midogo ,duh
Uwanja wa Emirate ,kiingilio chake , chukua cha OT mara mbili yake na sent kadhaa, ndio unaruhusiwa kuingia Emirates
Inaonesha unakichukulia poa poa Emirates ,
Ule uwanja ni wakisasa zaidi ya viwanja kama OT , NOU CAMP, uwanja wa madrid labda ,
Uwanja wa Emirates ndiyo wenye mpangilio mzuri zaidi ukilinganisha na viwanja vingi vya mpira hasa vile vinavyomilikiwa na timu kubwa.
Emirates ambao ulianza kujengwa na kukamilika Julai 2006 una mfumo wa kisasa zaidi kama utalinganisha na viwanja kama Old Trafford wa Manchester United au Stamford Bridge wa mabingwa wa England, Chelsea.
[
https://globalpublishers]
Mgahawa ndani ya Emirates.
Championi limefika katika viwanja vyote hivyo na Emirates unaonekana kuwa na ubora kuzidi ulivyo wa Camp Nou wa Barcelona na hata Santiago Bernabeu wa Real Madrid za Hispania, hasa unapozungumzia mpangilio wa ndani.
Kwa upande wa mashabiki ambao unaingiza hadi watu 60,432 waliokaa vitini, utaona aina ya ukaaji ni bora zaidi, viti vina nafasi ya mtu na mtu kwa maana ya mbele na nyuma, yaani sehemu ya kuweka miguu kama utalinganisha na Stamford Bridge au Old Trafford.
Ukaaji wake, yaani aina ya yai, inampa mtazamaji nafasi ya kufaidi zaidi mpira kwa kuwa mfumo wake umekuwa wa kisasa zaidi kuliko mtazamaji kukaa kama ananing’ng’inia kama ambavyo umekuwa ukiona kwenye Dimba la Camp Nou. Ukiingia Emirates utaona tofauti kubwa zaidi.
[
https://globalpublishers]
Sehemu ya kupata vinywaji na chakula ndani ya Uwanja wa Emirates.
Lakini ndani ya uwanja huo, kuna hoteli maalum ambayo unaweza kuuita ni mgahawa lakini ukawa na ubora kuliko hoteli za nyota tano za Ulaya au hata nyumbani Tanzania.
Ukiingia kwenye mgahawa wa Diamond, hakika kweli ni almasi namna ulivyopangiliwa na umegawanyishwa katika maeneo mawili. Moja likiwa ni kwa ajili ya watu maarufu tu ambao wanahusika na klabu hiyo au wageni wao. Lakini sehemu ya pili ni ile ambayo hutumia wateja waliolipa VIP.
Kunakuwa na chakula maalum ambacho huwekwa kwa mfumo wa “bufee” na wakati wa mapumziko au kabla na baada ya mechi, watu hujiachia wanavyotaka wao.
INGIA HAPA UUJUE ZAIDI UWANJA WA EMIRATES ,UACHE KUUFANANISHA NA VIWANJA VINGINE
Bata La Ndani Ya Emirates, Hakuna England - Global Publishers