Arsenal walala 2-1 mbele ya Everton

Arsenal walala 2-1 mbele ya Everton

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
_92961283_09a2f0a7-a959-4ed7-a215-69ec9a6efe95.jpg

Arsenal wamepoteza nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya Everton kutoka nyuma na kuondoka na ushindi wa 2-1.

Washika bunduki hao walishinda michezo mitatu mfululizo walianza vyema katika mchezo dhidi ya Everton baada ya Alexis Sanchez kupiga safi mkwaju wa adhabu nje kidogo ya eneo la hatari uliombabatiza mlinzi Ashley Williams na kuingia wavuni.

Everton walisawazisha na kuwa dakika chache kabla ya kwenda mapumzikoni baada ya Seamus Coleman kumalizia vyema mpira uliopigwa na mlinzi Leighton Baines.

_92961008_6351c7df-f6b9-484f-9e47-c332b2019ac8.jpg

Kipindi cha pili kila timu ilirejea kwa lengo la kuchukua alama tatu lakini ni Everton ndio waliofanikiwa baada ya Williams kufuta makosa yake kwa kuifungia Everton goli la pili na la ushindi.

Nahodha wa timu ya Everton Phil Jagielka alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache tu kabla ya kumalizika kwa mchezo huo baada kupata kadi ya pili ya njano.

_92961009_e7223f5a-9096-4b5c-9275-a6f1a0e6ee20.jpg

Kwa matokeo hayo Arsenal wanabaki nafasi ya pili wakiwa na alama 34 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya vinara Chelsea wenye alama 37.

Everton wanabakia nafasi ya saba wakiwa na alama 23.

Chanzo: BBC
 
safi sana asenane.hao ndo toffees bana. tulichekelea sub ya fellaini juzi juzi tu hapa,sasa leo nami nachekelea sub ya giroud kwikwi kwikwikwikwi
 
Hizi habari ni za uzushi so wanamichezo zipuuzeni
 
Back
Top Bottom