Arteta lazima abatizwe kwa Moto, kinachomkuta sasa kilitegemewa kabla hajasaini kufundisha Arsenal

Arteta lazima abatizwe kwa Moto, kinachomkuta sasa kilitegemewa kabla hajasaini kufundisha Arsenal

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Moja ya vitu ambavyo haviniumizi kichwa na moyo ni kufungwa kwa Arsenal kwa kipindi hiki ni kitu ambacho tayari nilishakifahamu.

Kutoka kwa Arsene Wenger mpaka kwa Unai Emery tayari kulikua na makosa mengi ambayo hayabadilishiki kwa kipindi kifupi, ni jambo la process na muda.

DESIRE YA ARTETA NI KUBWA KWENYE UFUNDISHAJI WAKE LAKINI VITENDEA KAZI AMEKOSA
Hapa nikimaanisha wachezaji waliopo asilimia kubwa wana viwango vya timu za kawaida badge ya Arsenal inawaelemea.

Ili tupate kile tunachohitaji hatupaswi kumlaumu au kumtukana Arteta bali honestly Arteta anahitaji madirisha manne au matatu ya usajili ili kuitengeneza Arsenal ya ushindani na kuogopeka.

Upande wa magolikipa sioni madhaifu kuanzia kwa Berd Leno, Emiliano Martinez mpaka kwa Mart Macey

MADHAIFU MAKUBWA YAPO KWENYE SAFU YA ULINZI NA SAFU YA KIUNGO HIZI SEHEMU ZINAHITAJIKA KUFUMULIWA ZOTE NA KUUNDWA UPYA

Je, tutafanikiwa kwenye hilo? Hapa inahitaji utimamu kwenye management ya timu mpaka kwenye benchi la ufundi.

TUANZE KUANGALIA KWENYE SAFU YA ULINZI
Hii ni moja ya sehemu ambayo inahitaji kufumuliwa kwa kiwango kikubwa na kwa utimamu zaidi.

Kwa chaguo langu mimi naweza kubakisha watu watatu tu kwenye safu ya ulinzi ambao ni PABLO MARI,CALUM CHAMBERS, BELLERIN pamoja na KIERAN TIERNEY hawa ndo watu wanaoonekana wana uwezo wa kupambana kwa ajili ya badge ya timu na pia tunahitaji watu sahihi wa kuwapa competition hao watu niliowataja hapo.

SEHEMU NYINGINE NI SEHEMU YA KIUNGO
Hapa ndo kwenye mtihani mkubwa sana na tuna mchezaji timamu mmoja tu kwenye sehemu hii ambae ni GRANIT XHAKA na pia tuna mtoto mmoja tu ambae akiamua kuwa mtu mzima basi atafanya makubwa kutokana na ufundi pamoja na spirit aliyo nayo hapa namzungumzia MATTEO GUENDOUZI ila hao wengine wote sidhani kama nisahihi kubaki pale.

Xhaka ni bora, timu ndo mbovu. Hata Pogba kuna kipindi alionekana mbovu kutokana na ubovu wa timu. Likewise Busquets anaonekana mbovu hivi sasa kutokana na ubovu wa timu.

Arsenal ni mbovu, tena mbovu mno, pale hata ukimleta Messi/Ronaldo akashika nafasi utamuona utopolo tu.

Timu inanuka uozo tangu miaka ya 2010 huko, wala tusiseme ni kutokana na mabadiliko ya kocha Arsenal ilikuwa mbovu tangu kitambo kuanzia Academy hadi Seniors.

Even Auba hadeserve kuwepo Arsenal, ninadhani anaona aibu kutuchana kutokana na nafasi yake ya u'Captain.

We are the shittiest among the top teams!

Sehemu hizo zikijengwa kwa utimamu na usahihi basi tutaiona ile Arsenal tunayoihitaji na Arsenal itakayoheshimika

NOTE: ARTETA NI MBUZI WA KAFARA NI LAZIMA ACHINJWE TU HALITOEPUKIKA JAMAA AMESAKIZIWA MBWA KICHAA
 
Naona Xhaka kucheza n Guendouz kulimmaliza. Maana alikua anaogopa kupanda na kumuachia yule mtoto dimba. Wote wakiwa nyuma Ozil anaonekana utumbo tu as hana ball winning kama ya Fabregas.

Mimi nakubaliana na wewe sehemu ya kusema tunahitaji kiungo. Na huyu Partey kama atakuja Xhaka itabidi aende as Torreira ni mzuri ana fighting spirit kubwa ball winning ipo pia. Guendouz afanyie kazi speed na stamina atakua hatari.

Mabeki waliopo siyo wabaya sana ila Luiz aende, Mustafi aende, Lacazete aende, Sokratis aende, Kolasinac. Damu changa itawale.

Kama inawezekana. Tumpate Coutinho, tuibembeleze Madrid ituachie Jovic hata kwa mkopo. Tumpate Partey, tumpate Upamecano.

Pepe goli aliloshinda siku ya mechi na Brighton wenzake left footed wingers ndiyo magoli yao kwahiyo aongeze juhudi au benchi limhusu.
 
Hii ni alert kwa viongozi wa juu kuwa wanatakiwa kufanya serious transformation especially kwa wachezaji.Sidhani kama hawajui kuendelea kuwa wasindikizaji hivi brand ya timu inashuka.Wafanye hivyo.
 
Guendouz hamna kitu pale alipo ndio mwisho wa uwezo wake
 
Arsenal ni kubwa sana kuliko wachezaji,yaani hakuna uwiano kati yao.....wachezaji waliopo 88% ni wakucheza championship, na hao 12% hawana watu wanaowapa changamoto, wanacheza bora liende bila presha,timu haipo sharp yaani wakiwa wanacheza hujui wanataka nini,
Ili hii timu irudi vizuri inahitaji misimu kadhaa ya msoto,

Tupo na Tutakuwepo

COYG
 
Tatizo lake hajui kupiga krosi. Tierney ni expert kulko yeye
Hiyo ndiyo kazi ya kocha msaidizi wa Arteta hasa wa ufundi kumboresha Kolasinac kama vile Arteta alivyomsaidia Pep Guardiola kuwafua akina Raheem Sterling, au kama vile Pep Lijnders anavyomsaidia Klopp kuwafua akina Trent au Hernderson hadi wanajua kupiga long balls, crosses kama De Bruyne.
 
Back
Top Bottom