bht nakubaliana na wewe kabisa kuwa uamuzi aliouchukua mke si sahihi lakini tukumbuke kuwa watu tunatofautiana jinsi ya kureact.nadhani the boss aliniuliza kitu nikamweleza ingekuwa mimi ningereact tofauti kabisa (ingekuwa mimi) lakini si wote wenye guts za kureact kama unavyofikiria wewe mpenzi. Kuna circumstances kibao, mwingiine anafikiria watoto wake (kama wana watoto); mwingine jamii tu inam-scare hata kufikiria uamuzi kama wa kukatisha mkataba wa ndoa. Kwa huyu dada inawezekana kabisa kuwa anafall kwenye mojawapo ya makundi haya ili mradi tu anao uwoga wa kuvunja ndoa. Najua wapo watakaoniuliza kama anaogopa kuvunja ndoa why akafanye kitendo ambacho ni dhahiri kinnawezapelekea kuivunja hiyo ndoa ambayo anajitetea kuiprotect ?? Well kuna post ambayo ameiweka mbu juu ya kutafuta faraja..........nadhani hii ilikuwa ni process
si kwamba ameamka, akavaa akatoka akaenda barabarani akasimama na kumpata mshefa la hasha. Si ajabu mshefa ni mtu wa karibu sana na familia yake, na pengine ni mtu ambaye yeye alianza kumweleza matatizo yake (kama rafiki either wa familia au rafiki tu) akawa anafarijiwa (si kimapenzi) hata ile kusikilizwa akilitoa dukuduku lake then in the process pengine ikafikia kulia, kubembelezwa, kukumbatiwa na mwisho kukissiwa na baadae kuliwazwa.
Yeye kama mwathirika kweli tutamhukumu kwa kushindwa kujizuia kipindi akiwa vulnerable?? Hebu tuangalie kwa upande huu pia jamani tuache kumnyooshea vidole mmama wa watu ambaye ameshagundua kosa sasa anataka kuweka sawa mambo.
mtm na fide ninaomba niwaulize swali la nyongeza: Suppose huyu mdada angekuja hapa akiomba ushauri wa manyanyaso na abuses anazozipata toka kwa mumewe; kunyimwa haki ya ndoa, kupigwa, mume kulala nje, mngemshaurije??