Arudisheje hisia kwa mumewe? ...Msaada tafadhali

sasa huyu dada ndio aliona ndio njia mbadala ya kupunguzia machungu yake, na ndio kashanogewa hivyo so kifutacho ni kuishi na mume kwa ajili ya watoto, mume alichokuwa anakitafuta amekipata.....

Nini sasa suruhisho la hii ndoa?

They need something special that's why they do it.

Hapa mkuu linakuja swala la kwa vile yeye anafanya ngoja na mm nifanye sijui ukifanya kwa kulipiza kwa ubaya unamkomoa nani.

Well said mkuu

Kama mtu unafanya kwasababu fulani alifanya basi hapo ni confirmed kwamba UPUMBAVU UMEZIDI UJAZO.....mtu Unapofanya unatakiwa kufanya kwa utashi wako na sio kwasbabu partner kafanya

Anyway

Kumsaidia "shogake" MJ1, mwambie aendelee hadi mafuta yatakapoisha then atajua cha kufanya!!! Kwani hainiingii akilini mtu anataka kuacha halafu anshindwa, hapo ndio huwa sielewi, ukiamua kuacha unaacha.... ukiamua kuendelea unaendelea

Reactions: bht
what about cheating for fun, as NN showed how it is done in the US

Cheating is cheating and it has no geographical boundaries with regards to the reason(s). If you study carefully the reasons of why people cheat you will see that they are always very similar in nature.

ndo maana mimi nimesema na ninasema tena dada hajaamua kuacha, na kama ni hivo sisi ni nani basi hata tumwambie aache kama nafsi yake haijakubali?!!

Huyo anatafuta sababu tu. Anadanganywa na fedha ndiyo maana hataki kurudi kwa mume wake!

Kumsaidia "shogake" MJ1, mwambie aendelee hadi mafuta yatakapoisha then atajua cha kufanya!!! Kwani hainiingii akilini mtu anataka kuacha halafu anshindwa, hapo ndio huwa sielewi, ukiamua kuacha unaacha.... ukiamua kuendelea unaendelea

Shoga ake MJ1 hilo lishefa linamdanganya tu nalo imradi siku zipite.
Nacho ona hapo shoga ake MJ1 amepata kitu ambacho hakukipata kwa mmewe ndo maana ameamua kumganda mshefa.
Lakini anaweza kufanya maamuzi magumu akarudi kuimarisha ndoa yake kwa kukaangalia wapi alijikwaa.

ndo maana mimi nimesema na ninasema tena dada hajaamua kuacha, na kama ni hivo sisi ni nani basi hata tumwambie aache kama nafsi yake haijakubali?!!

Kama hajaamua kuacha basi aombe aolewe aone kama mshefa yupo tayari kubeba mizigo miwili kwa wakati mmoja.
Wanawake ni wepesi sana kudanganyika na mianaume inayo kata kiu kwa muda tu

Nini sasa suruhisho la hii ndoa?

Suluhisho wanalijua wao wahusika. Suluhisho litakalonifaa mimi au wewe huenda kwake au kwao likawa lisiwa suluhisho.

Sasa kwa mtu kama mimi, kwangu suluhisho ni "usinijue" kabisa. Huwezi ukanidhalilisha namna hiyo halafu eti uje unajiliza liza nikusamehe. Ila kwa manufaa ya haki, kama na mimi niliwahi kumtenda hapo labda nitafikiria kusamehe. Lakini kama sikuwa sijamtenda halafu nikajua kuwa kanitenda basi na ajue huo uhusiano ni mfu.

Wengine sisi tuna -30 tolerance kwenye mambo haya.

Hapo sijaona bado mkimsaidia jinsi ya kuondoa feelings zake kwa mshefa .................siku hizi ushauri umegeuka lawama sishangai kuona hata relationship nyingi zikiingia shimoni sababu ya lawama.......watu wamekuwa hata waoga kusema yaliyo mioyoni mwao maana mwisho wa siku ni vidole juu ya vidole ndio tunaishia kutengeneza nidhamu za uoga.

Kama hajaamua kuacha basi aombe aolewe aone kama mshefa yupo tayari kubeba mizigo miwili kwa wakati mmoja.

Wanawake ni wepesi sana kudanganyika na mianaume inayo kata kiu kwa muda tu

Fide kuna uwezekano wa ndoa hapo unavoona wewe?

Aksante sana Kipimapembe...huu mchango wako nimeupenda angalau umetoa mapendekezo ya hatua muhimu ambazo anawezazifuata ili afanikiwe kuachana na huyu Mshefa. Ila tu kama walivyosema wadau wengine kuwa cha muhimu ni kuwa awe na dhamira madhubuti kuwa ameamua kuachana kiukweli na ameamua kuipigania na kuilinda ndoa yake.

Ubarikiwe sana Kipima pembe

Hili sredi bado linaendelea?

Kama vipi nianze kulichakachua............ Sredi likiwa siriaz mwanzo mwisho linatakiwa lihamishiwe jukwaa la siasa.

MJ1 Msalimie shoga yako........BTW huyo mshefa wake unamjua?..........Navyowajua wanawake ntashangaa kama hajakuonyesha mtuwe kama kweli ni shoga yako kivile.....

.Habari zenu waungwana.......... nlikuwa napita tu, narudi jukwaa pendwa la maria roza.

hivi mnajuaje kama huyu dada alifanya revenge au alifanya coz kama binadamu kamili anahitaji kitimiziwa hilo hitaji?

Hata mimi nimejiuliza hivyo hivyo.

Lakini kwa vile tunaambiwa eti 'mwanamke hawezi kucheat bila sababu' (whatever the hell that means) basi eti lazima mumewe ndo atakuwa kampa hiyo sababu.

Sasa mimi nashindwa kuelewa. Kwani kucheat kwa sababu ya tamaa yenyewe si sababu hadi sababu isababishwe na mume? Haiingii kichwani kabisa.

Dearest, binafsi nahisi naongeza mateso juu ya mateso. Ni either nijaribu kutimiza wajibu wangu kurejesha afya kwenye mahusiano yetu au nikayafanye hayo nikijua basi mkata wetu umeisha....

bht nakubaliana na wewe kabisa kuwa uamuzi aliouchukua mke si sahihi lakini tukumbuke kuwa watu tunatofautiana jinsi ya kureact.nadhani The Boss aliniuliza kitu nikamweleza ingekuwa mimi ningereact tofauti kabisa (Ingekuwa MIMI) lakini si wote wenye guts za kureact kama unavyofikiria wewe mpenzi. Kuna circumstances kibao, mwingiine anafikiria watoto wake (kama wana watoto); mwingine jamii tu inam-scare hata kufikiria uamuzi kama wa kukatisha mkataba wa ndoa. Kwa huyu dada inawezekana kabisa kuwa anafall kwenye mojawapo ya makundi haya ili mradi tu anao uwoga wa kuvunja ndoa. Najua wapo watakaoniuliza kama anaogopa kuvunja ndoa why akafanye kitendo ambacho ni dhahiri kinnawezapelekea kuivunja hiyo ndoa ambayo anajitetea kuiprotect ?? well kuna post ambayo ameiweka Mbu juu ya kutafuta faraja..........nadhani hii ilikuwa ni process

Si kwamba ameamka, akavaa akatoka akaenda barabarani akasimama na kumpata mshefa la hasha. Si ajabu Mshefa ni mtu wa karibu sana na familia yake, na pengine ni mtu ambaye yeye alianza kumweleza matatizo yake (kama rafiki either wa familia au rafiki tu) akawa anafarijiwa (si kimapenzi) hata ile kusikilizwa akilitoa dukuduku lake then in the process pengine ikafikia kulia, kubembelezwa, kukumbatiwa na mwisho kukissiwa na baadae KULIWAZWA.

Yeye kama mwathirika kweli tutamhukumu kwa kushindwa kujizuia kipindi akiwa vulnerable?? Hebu tuangalie kwa upande huu pia jamani tuache kumnyooshea vidole mmama wa watu ambaye ameshagundua kosa sasa anataka kuweka sawa mambo.

MTM na Fide ninaomba niwaulize swali la nyongeza: Suppose huyu mdada angekuja hapa akiomba ushauri wa manyanyaso na abuses anazozipata toka kwa mumewe; kunyimwa haki ya ndoa, kupigwa, mume kulala nje, mngemshaurije??

Dunia haijaharibika ila binadamu ndio walio haribika. Inawezekana vipi upo ndani ya ndoa kisha unaendeleza uzinzi! Inawezekana ndoa nyingi hufungwa kwa matamanio tu badala upendo wa dhati unaotoka moyoni mwako. Ila ukiwa na upendo wa machoni, huo hauitwi upendo bali ni matamanio.

So matamanio unapokuja kuyageuza na kuwa upendo, ndipo uaminifu ndani ya ndoa unapotoweka coz yale matamanio ambayo alikuwanayo kwako au kwake yameisha huenda yamehamia kwa mwingine. Inatakiwa tubadirike tukiamuwa inawezekana.

We nae hebu rudi kitandani kwako!!
Babu kwenye mMain thread inasema ni rafiki yetu kifamilia (Family friend) na si shogaangu! Ni mtu ninayemuheshimu. Kama sikuwahi kuhisi achilia mbali kujua kama ana-mshefa, ningeonyeshwa saa ngapi?

MJ1 samahani kama nimeonekana kumnyooshea saana dada kidole. na pia sikutaka yeye awe mimi au mtu mwingine yeyote humu na kamwe hatutafana.

pointi yangu ya mkazi imekuwa dada aamue mwenyewe kubadilika na si vinginevyo. sisi tutashauri ahame mji, abadili simu, amwambie mume amsaidie kumkanya mshefa, nk. lakini mwamuzi wa mwisho ni yeye tu. kinyume na hapo ndo tunaishia kuishi maisha ya maigizo kwa sababu jamii ndo inatutaka tuishi hivo (sio sisi tutakavyo tena)

samahani tena lakini yote yalikuwa ni katika kupanua uwanja wa majadiliano ili tupate suluhisho la tatizo.

....vumilia.......

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…