Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wananchi wa kata ya kiutu wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha wameandamana na kufanya kikao na Diwani wao wa kata hiyo Malaki Marambo Kwa lengo la kushinikiza kumkataa Mwenyekiti wao Hashim Saitabao aliyeshinda uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024
Chanzo Cha wananchi hao kumkataa Saitabao inadaiwa kuwa ni baada ya Mwenyekiti huyo kumpiga mwananchi anayefahamika kwa jina la Julias Ngoishilo kwa kutumia fimbo aina ya rungu eneo la kichwani na kumvunja mkono
Aidha wananchi hao wamemuomba diwani huyo kuweza kuwaletea Mwenyekiti mwingine ambae atashikamana na wananchi katika mambo yote ya jamii.