Chama cha
@actwazalendo_official kimeshinda uenyekiti wa kijiji cha Nkoasenga kilichoko Kata ya Leguriki Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha, kwa kura 528 dhidi ya kura 418 za CCM, zilizotokana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Hivyo basi, aliyekuwa mgombea wake, Jotsun Mbise ndiye mwenyekiti mpya wa kijiji hicho.