Arusha: Chui, fisi tishio kwa mifugo

Arusha: Chui, fisi tishio kwa mifugo

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Wakazi wa Ngorongoro wameeleza kuishi kwa mashaka katika makazi yao kutokana na uwepo wa wanyama wakali ambao wamekuwa wakila mifugo yao.

Uwepo wa wanyama kama Chui na Fisi unatajwa pia kuwatia hofu wazazi pindi watoto wao wanapoenda na kurudi shuleni ambako hulazimika kutembea umbali kati ya km 5 hadi 15.

Wakati hayo yakijiri Ngorongoro, katika Kijiji cha Msomera ambapo wananchi zaidi ya 500 kutoka Ngorongoro waliohamia kwa hiari hofu ya wanyama haipo tena .

Kutokana na hali hiyo kunatajwa uwepo wa Ombwe kwa kundi la wananchi katika eneo la Hifadhi ya Ngorogoro kuhama na kwenda sehemu watakayokuwa huru bila hofu ya wanyama wakali.

CHANZO: Clouds TV
 
Population inapopungua, kukawa na ukimya, wanyama huongezeka, kwa sababu wameambiwa wahame bora wahame.
 
Wanyama wanajua ndo maana hata nyumba yako ikiwa karibu na kichaka au pori hutakiwa kuacha bila ya mtu hata kwa wiki .

Ukifunga nyumba ikiwa kimya bila ya mtu unaweza kukuta nyoka kama chatu yupo ndani au mnyama wowote mpaka unajiuliza katokea wapi.
 
Wanafugaje bila kinga/ulinzi shirikishi dhidi ya fisi na chui.
 
Back
Top Bottom