LGE2024 Arusha: Godbless Lema awatimua Maofisa wa TAKUKURU kwenye semina ya Wagombea wa CHADEMA, adai Wameacha uozo ufanywe kwenye Uandikishaji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Nabii wa Mungu, Godbless Lema, leo amekitendea haki Cheo Chake cha Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, baada kuwatimulia mbali Maofisa wa TAKUKURU waliohudhuria semina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali za Mitaa.

Nabii Lema ambaye Unabii wake juu ya Mambo kadhaa ya Tanzania Umetimia na kupitiliza, amewaambia Maofisa hao wa TAKUKURU kwamba Wameacha uozo kwenye Uandikishaji uliofanywa na viongozi wa serikali halafu wanakimbilia kuleta pua zao kwenye Semina zisizo na Makando kando za Chadema.

Screenshot_2024-11-07-19-58-43-1.png
Screenshot_2024-11-07-19-58-53-1.png
Screenshot_2024-11-07-19-59-01-1.png

Binafsi Naunga Mkono Jambo hili

=====

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema amewafukuza maofisa watatu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwenye semina ya wagombea wa wenyeviti wa mitaa wa chama hicho.

Lema aliyekuwa mgeni rasmi leo Novemba 7, 2024 katika mkutano huo jijini Arusha, baada ya kuingia ukumbini na kupata utambulisho kuhusu uwepo wa maofisa wa Takukuru waliokuwa meza kuu, alisimama na kusema hakubaliani na uwepo wao.

"Sitakubali muongee na wajumbe wetu wakati mmeshindwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wa serikali wakiwemo wasimamizi wa uchaguzi na wasaidizi wao pia waandikishaji wa daftari la wapiga kura kwa vitendo walivyokuwa wanafanya hivyo naombeni muondoke hatuwahitaji hapa,”alisema Lema.

Hata hivyo maofisa hao waliokuwa wamekaa meza za mbele kwa wageni rasmi hawakunyanyuka hadi wasimamizi wa ulinzi wa semina hiyo walivyowafuata na kuwanyanyua kwa nguvu ndipo wakaamua kutoka huku wakizomewa na ukumbi mzima.

Akizungumzia hali hiyo, kwa njia ya simu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo amesema suala hilo si jema lakini haliwezi kuzuia elimu ya rushwa kuwafikia wananchi.

Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi
 
Nabii wa Mungu, Godbless Lema, leo amekitendea haki Cheo Chake cha Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, baada kuwatimulia mbali Maofisa wa TAKUKURU waliohudhuria semina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali za Mitaa.

Nabii Lema ambaye Unabii wake juu ya Mambo kadhaa ya Tanzania Umetimia na kupitiliza, amewaambia Maofisa hao wa TAKUKURU kwamba Wameacha uozo kwenye Uandikishaji uliofanywa na viongozi wa serikali halafu wanakimbilia kuleta pua zao kwenye Semina zisizo na Makando kando za Chadema.

View attachment 3146379View attachment 3146382View attachment 3146387View attachment 3146388

Binafsi Naunga Mkono Jambo hili
Cha kina drama sana hiki hakina mambo ya maana zaidi ya upuuzi na utoto!
 
Safi Lema,wapuuzi sana hao TAKUKURU,watoto wa shule wa miaka 15 wanaandikishwa kama wapiga kura wenyewe wanajifanya hawaoni,wamekaa wanatafuna sambusa ofisini halafu wanakuja kujisafishia kwenye vikao vya Chadema
 
Nabii wa Mungu, Godbless Lema, leo amekitendea haki Cheo Chake cha Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, baada kuwatimulia mbali Maofisa wa TAKUKURU waliohudhuria semina ya Wagombea wa Uenyekiti wa Serikali za Mitaa.

Nabii Lema ambaye Unabii wake juu ya Mambo kadhaa ya Tanzania Umetimia na kupitiliza, amewaambia Maofisa hao wa TAKUKURU kwamba Wameacha uozo kwenye Uandikishaji uliofanywa na viongozi wa serikali halafu wanakimbilia kuleta pua zao kwenye Semina zisizo na Makando kando za Chadema.

View attachment 3146379View attachment 3146382View attachment 3146387View attachment 3146388

Binafsi Naunga Mkono Jambo hili
Huyu dogo wa kati ninamfahamu ni mnoko hatari
 
hivi ni kweli nae Lema ameacha unyang'anyi wa malori ya watu huko misituni au sasa hivi anatuma makamanda na nabii anapokea mahesabu tu?

Ila nabii kachoka sana dah? Kulikoni 🐒
 
Tuwajue wakurugenzi DED wasimamizi wakuu wa uchaguzi serikali za mitaa wanaowajibika kusimamia haki katika mchakato wa uchaguzi na wale ambao wanashiriki na kufumbia macho uchafuzi wa uchaguzi wa 2024

1731002814583.jpeg
 
SIO JAMBO LA KIUNGWANA.
HII INAMAANISHA ANAUNGA MKONO MATENDO YA RUSHWA.ITAWAGHARIMU CHADEMA KWENYE CHAGUZI
Kwamba hao Takukuru ni kweli wanapambana na rushwa? Itawagharimu cdm kwa kipi, kwani kuna uchaguzi serious hadi useme itawagharimu cdm? Hao Takukuru ni taasisi ya kulinda wala rushwa nchi hii, na Lema amefanya jambo sahihi kuwafukuza.
 
Itundikwe Listi ya taasisi na ma DED wa Halmashauri walioshindwa kusimamia haki uchaguzi wa 2024, maana tunaelekea 2025.

Tunalipa kodi bila ubaguzi wa huyu chama kile yule hiki, halafu inapokuja uchaguzi wanatumia kodi zetu bila aibu kwa Taasisi za umma na vigogo kama maDED kuanza kubaguana kutimiza wajibu wa taasisi zao kusimamia haki na demokrasia bila kusahau 4R

Name and shame list :
 
Back
Top Bottom