Arusha imekuja kuwaje? Mkoa Mzuri Ila Jamii Inaangamia

Na hao wanaosemwa ni mashoga wa tour guide nao una maoni gani?
 
Kwani Arusha ina sifa gani nzuri kuhusu vijana wake?
Haina. Hakuna wakazi wa mkoa flani wenye sifa ya kipekee. Mawazo ya namna hii yanatokana na uzushi na mazoea tu yenye ukabila, udini nk.

Msimamo wangu ni kwamba hakuna sehemu Tanzania isiyo na matatizo, na wananchi wameshazoea kwasababu hakuna mbadala.

Ingekuwa Arusha haifai kweli basi hilo tungeliona wazi mfano watu kuhama, matukio ya kutisha, viongozi kujiuzuru nk.
 
Rafiki zangu walivyokuwa wanausifia mkoa wao na nilichoenda na kukikuta ,itoshe kusema tu vimikoa vya Tanzania ni takataka.
 
Kwahiyo unataka kusema watu wa Tanga ni wazushi wanaposifiwa ni wataalamu wa mapenzi? Au wachaga ni wapambanaji na wafanya biashara wazuri?

Hatukatai kila mkoa haukosi matatizo lakini huoni km sehemu nyingine yamezidiana?
 
Kwahiyo unataka kusema watu wa Tanga ni wazushi wanaposifiwa ni wataalamu wa mapenzi? Au wachaga ni wapambanaji na wafanya biashara wazuri?

Hatukatai kila mkoa haukosi matatizo lakini huoni km sehemu nyingine yamezidiana?
Kuna kuamini, halafu kuna kujua. Je, tunaweza kuthibitisha kwamba asilimia kubwa ya wachaga ni wafanyabiashara wazuri ama watanga ni wafanyamapenzi wabobevu? Hapana.

Kitakwimu, mkoa wa kipolisi wa kinondoni ndiyo unaoongoza kwa kesi za uhalifu nchini.

Zile tamaduni za vijana wa arusha kama lafudhi na kujisifia uhuni ndio zinafanya watu waamini mkoa mzima unatisha.

Kuna watu zaidi ya milioni 2 kule na wanaendesha shughuli zao vizuri tu. Uhalifu upo ila sio kwa kiwango kinachosadikiwa.
 
Arusha na Moshi ilikuwa inaongoza kwa matukio ya ujambazi miaka ya nyuma. Nafikiri hii ndio imepelekea mpaka leo huo mkoa kuonekana una uhalifu na vijana wake wakiwa wamebeba hiyo dhana ya ukauzu, ubabe na ujuaji..!!

Wachaga wanaweza wasiwe wote wafanyabiashara lakini wengi wao ni wapambanaji kutokana na sifa yao ya kuishi mkoa wowote Tanzania na kufanya maendeleo..!!

Kila mkoa ina sifa nzuri na sifa mbaya japo maeneo mengine yamezidiana..!!
 
Umesahau kuwataja WADUDU. Yaani imekuwa ndiyo icon ya Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…