Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 753
- 1,812
Kesi ya Mgogoro wa Ardhi baina ya Kanisa la Christ Synagogue Ministries lililopo Sakina jijini Arusha na wasimamizi wa mirathi Bernadette Changuru na Samweli Changuru inatarajia kuanza kusikilizwa Desemba 6, mwaka huu.
Shauri hilo namba 57/2021 linasikikizwa na Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Arusha, Mbele ya mwenyekiti wa Baraza hilo, Gladness Kagaluki ambapo mwishoni mwa wiki lilikuja mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa terehe ya kusikilizwa
Wakili wa upande wa mashtaka, Ismael Shallua alieleza mahakama hiyo kwamba shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa ,hata hivyo upande wa wajibu maombi ukiwakilishwa na Wakili Gwakisa Sambo walidai wapo tayari Kwa hatua za usikilizwaji .
"Mheshimiwa mwenyekiti shauri hili limekuja Kwa ajili ya kutajwa tulikuwa tunaomba muda mwingine Kwa ajili ya kusikilizwa"alisema Wakili Shallua
Mwenyekiti wa Baraza hilo, Kagaluki aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 6,mwaka huu saa tano asubuhi litakapokuja kwa ajili ya kusikiliza.
Wakati huo huo shauri dogo namba 199/2021 lililofunguliwa na mlalamikaji ambaye ni Kanisa la Christ Synagogue Ministries akipinga kuondolewa katika eneo linalobishaniwa, limeahirishwa hadi Septembe 13 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Baraza hilo la Ardhi na Nyumba, Hakimu, Kagaluki alidai kuwa baada ya makubaliano ya pande mbili kuwa shauri hilo litaendeshwa Kwa majibizano ya barua,ifikapo Septembe 13 mwaka huu litakuja mahakamani hapo kwa ajili ya kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.
Nje ya mahakama Msimamizi wa mirathi, Bernadette Changuru Mkazi wa Mbauda jijini Arusha,ambaye ni mke wa marehemu Silas Chunguru aliyefariki mwaka 2019 ,aliliomba Baraza hilo kuharakishwa Kwa kesi hiyo na kuacha kupanga tarehe za mbali ili haki iweze kutendeka haraka Kwa kuwa yeye ni Mjane.
Katika shauri hilo,Nabii Odilo wa kanisa Hilo alifungua shauri dogo katika mahakama hiyo kupinga kuondolewa na msimamizi wa mirathi katika eneo ambalo alipangishwa na kujenga kanisa.
Pia Nabii huyo alifungua kesi katika mahakama hiyo alidai eneo hilo ni Mali yake aliuziwa na marehemu Jambo ambalo si kweli .